
Wakati mwingine una weza kusema ni hadithi kwa mke na mume kufa kwa wakati mmoja Eliki Kayombo alimua mkewe kwa kumtwanga na mpini wa shoka na Paulina kufariki papo hapo katika kijiji cha Sanangula kata ya tanga, Mtoto Alana kayombo akiwa na furaha bila kujua kilicho tokea

Hawa hapa juu wameingia katika maisha ya mazingira hatarishi bila kupenda ni watoto wa Eriki Kayomb ambaye baada ya kumua mkewe naye alijinyonga nyuma ya nyumba yake kwa kugombea shuka. kutoka kushoto ni Rubeti Kayombo anaye fuatia letisia kayombo na wa mwisho ni Hepy kayombo

Aliye vaa suti nyeusi ni Afisa Mtendaji wa kijiji cha sanangula ambaye mpaka sasa mzigo mkubwa ume baki kwake kuwa tunza hao watoto katika kuadhimisha siku ya ukatili wa kijinsia mheshimiwa Jenista Mhagama aliwa changia watoto hao shilingi 50,000 na mwenyekiti wa uwt mkoa Kurusumu Mhagama naye alichangia shilingi 3000/=

Jamani watoto hawa wana hitaji msaada wa Jamii hawana ndugu wala Rafiki tuwachangie ili wasome waishi vizuri ,Mtoto mmoja Mheshimiwa Jenista Mhagama amejitolea kumsomesha jee sisi tuna fanyaje ?
No comments:
Post a Comment