
Waumini wa Dhehebu la Lutherani wakiwa katika Ibada ya Krismas Mjini Songea

Wanakwaya wa Kanisa la Lutherani wakifurahia kuzaliwa kwa Mkombozi wao Yesu Kristo ikiwa ni ishara ya upendo na ukombozi kwao katika Ibada ya Sikukuu ya Krismas.

Wachungaji wa Kanisa la Lutherani wakifurahia tunu zilizokuwa zikitolewa na waumini wao ikiwa ni ishara ya Upendo kwa kujiwa na Mkombozi wao Yesu Kristo

Watoto wa Kipapa wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Songea wakiwa katika Ibada ya Krismas kanisa la mtakatifu Matias Mlumba Kalemba

Padri na wahudumu wakiwa katika Misa Takatifu ya Krismas katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Matias Mlumba Kalemba Jimbo la Songea

Mchungaji John Msyani wa Kanisa la Moraviani akisisitiza kuendeleza Upendo kwa waumini wa Kanisa la Moraviani katika kusherekea Sikuu ya kuzaliwa kwa Yesu.

Waumini wa Kanisa la Moraviani wakisikiliza kwa makini mahubiri mazuri ya Mchungaji John Msyani katika Ibada ya Sikukuu ya Krismas katika kanisa la Moraviani Songea Manispaa.
Waumini wanafunzi wa Sekondari ya wasichana Songea wakifuatilia kwa usikivu mkubwa Ibada ya Krismas katika Kanisa la Moraviani Songea Manispaa.
No comments:
Post a Comment