KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, June 29, 2013

NDOA NYINGI HIVI SASA ZINA VUNJIKA KUTOKANA NA UTAMADUNI WA KIGENI

Ndugu mtazamaji na msomaji wa Blog hii napenda kukupa kitu kipya ambacho huenda huja kifikilia au kukiwaza. Kwa utafiti nilio ufanya kwa kutembea nchi za Afrika mashariki na ya kati imeonyesha kuwa ndoa nyingi zina vunjika kutokana na kukosa mawasiliano kati ya mama na baba wakati wa kupumuzika usiku,

Naomba nikurudishe utafiti nilio fanya ndoa za vijijini kwa asilimia 25% zina vunjika kwa sababu ya tabia. lakini ndoa asilimia 80% kwa watu wanao kaa mjini ni ukosefu wa mawasiliano ya kimwili, Hebu ona ukubwa wa kinda hicho wana lala watu wawili wakigombana kila mmoja ana lala kwakwe jee mahusiano yana weza kurudi kwa mtindo huo.

Nirudi vijijini kuna vitanda vina itwa Teremuka Tukaze Vitanda hivi vime kuwa chanzo cha suluhisho la ndoa mtu akigombana na mke wake wakija kulala wote hutumbukia kwenye kitanda na tofauti zao zina anza kwisha toka wakati huo. Hivyo tujue Ukiwa na kitanda cha 6x6 .5x6, ujue ndoa yaklo una iweka Hatarini Jaribu kufanya ufumbuzi mara moja ili ndoa yako idumu, Hayo nimawazo yangu mimi niliyo ya tafiti kwa kipindi cha miaka 30 samahani sikipata kitanda cha Teremuka tukaze ni kikipata nita weka ili ulinganishe na mawazo yangu

Monday, June 17, 2013

UTALI WA NDANI ULIOPO KATA YA LIULI WA PASWA KUENZIWA NA WATANZANIA WENYEWE

Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
 Viongozi wandamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali la RUNECISO wakielekea Katika Jiwe la Pomonda kuona hali ya Pamgo lilipo katika Jiwe hilo ambalo lilihifadhi watu waliojificha wakati wa Vita vya 1 na vya 2 vya Dunia
 Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
 Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
 Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
 Katibu Muhtasi wa RUNECISO akiwa katika utalii nyuma ya Jiwe hilo la Pomonda eneo la Ziwa Nyasa akichukua kumbukumbu za Historia ya eneo hilo na Mabadiliko yaliyopo pembeni kushoto kwake ni mti ambao una umri zaidi ya karne moja lakini haukui zaidi ya hapo.
 Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
 Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
 Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Viongozi waandamizi wa RUNECISO hapo wakiwa ndani ya Jiwe hilo la kihistoria na kivutio cha watalii, picha unayoiona ni ndani ya pango la Pomonda ambalo lina uwezo wa kuhifadhi watu zaidi ya 250 kwa wakati mmoja lililotumiwa kujificha wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambapo wazalendo wa Kitanzania walikuwa wanajificha. Aliyekaa Chini ni Makamu Mwenyekiti wa RUNECISO na Mwandishi wa Star Tv akiwa amechoka baada ya kupanda kwa shida jiwe hilo hadi kulifikia Pango.
Hizi ni  Nyumba zilizopo katika ufukwe wa Ziwa Nyasa za wakazi wa kawaida wanaofaidi Ufukwe wa Ziwa Nyasa.
Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100,pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . Hapo Mwandishi wa Habari Adam Nindi baada ya Kuzunguka katika kulifikia pango hilo inaonyesha jinsi gani alivyochoka akiwa amelala chini. Nilimnukuu akisema "ukistaajabu ya Mussa Utaona na ya Firauni" Nilipomuuliza una maana gani alisema katika maisha yake hakutegemea na wala hakufikiria kama kunaweza kuwa na Pango zuri la kitalii katika Tanzania hii kama hili lililopo eneo la Ziwa Nyasa.
Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo.

RUNECISO YA FANYA MDAHALO KUHUSU MABADILIKO YA HALI YA HEWA KATIKA KATA YA LIULI WILAYA YA NYASA

Mkurugenzi wa Pomonda Raha Beach Joseph Ndomondo akitoa akichangia mada ya Mabadiliko ya hali ya hewa katika mdahalo ulio andaliwa na RUNECISO na kufadhiliwa na The Foundation Civil Society  ulio fanyika katika kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa
 Makamu Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Mbinga akifungua Mdahalo na Kukemea vikali kuhusu uvuvi samaki katika ziwa Nyasa  kutumia sumu, Pia amekemea kujisaidia Vikani na Ziwanina kumtaka kilaMwana kaya  kuwa na Choo
 Washiriki wa Mdahalo wa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wakiji funza kwa vitendo jinsi ya kutunza mazingira kati mwambao wa ziwa nyasa eneo la liuli
 Mwenyeki wa Mtandao  Police wanawake akishiriki  mdahalo wa  Mabadiliko ya Hali ya Hewa Liuli
Kaimu  OCD wa wilaya ya Nyasa wa kwanza kulia akisikiliza kwa makini mdahalo wa Madiliko ya Hali ya Hewa ulio fanyika Liuli
 Mwenyekiti wa RUNECISO Michael Mahecha akitoa neno la mbele na kuwa taka wananchi wa Liuli kuacha kuuza eneo la Ufukwe huko ni kuji tia umasikini.
ASS/INSP Fadhila Chacha akito mada kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa kwa kuwa taka Wananchi wa Liuli kuto fanya vitu kwa makusudi huku wakijua wa na Haribu Mazigira na kusababisha Mabadiliko ya hali ya Hewa
 Wadau wa Mdahalo wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa kisikiliza kwa makini mada Hizo kulia ni Katibu wa Ruvuma Press Mosses Konara
 Wadau wa Mdahalo Liuli wa kiratibu maswala mhimu katika mdalo huo, Ikiwemo kuorodhesha wavuvi wote wanao tumia sumu katika uvuvi,Wachomaji Moto ovyo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa na kuweka mikakati imara ya kukabiliana na vitendo hivyo
Washiriki wakiwa katika ziwa Nyasa kujifunza Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya navyo weza kuchangia uchafuzi wa mazingira

JESHI LA POLICE SONGEA LA KAMATA MENO 18 TEMBO NA NOTI BANDIA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deudedit Nsimeki akiwa ameshikaNoti bandia ambazo zime kamatwa wakati wa kuuza mahindi katika soko la sodeko manspaa ya songea
 Hyo nimeno ya tembo ambayo yamekamatwa katika kijijicha hanga yakiwa meno 18 ambayo yalikuwa yakisafirishwa kwenda Dar es salaam
 ona watu walivyo kuwa hawana huruma hayo ni meno ya tembo wadogo ambao walikuwa wakitegemewa kuwa wata kuwa rasilimali ya taifa lakini masikini wawindaji haramu wame katisha maisha ya tembo hao
 Noti bandia zilizo kamatwa manspaa ya songea katika soko la Sodeko, kwa mjibu wa kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Amesema kuzijua noti hizo ni kulingana kwa namba pia noti zina kuwa nyepesi
 Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata Vipande 18 vya Meno ya Tembo vikiwa kwenye Mfuko wa Salfeti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amefanikisha kukamatwa kwa meno ya Tembo vipande 18 vikiwa kwenye Mfuko wa Salfeti maeneo ya Hanga Misheni wilaya ya Namtumbo.

Wednesday, June 5, 2013

TUSIPO ANGALIA TUTAPOTEZA MAADILIYA UTAMADUNI WA WATU WA RUVUMA

 Hivi karibuni nilizungumzia kuhusu kupotea kwa lugha ya Asili kwa karine chache zijazo. Hebu sasa nizungumze kuhusu Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma. Hasa kuhusu Utamaduni wetu.
Tuna Ngoma za kila aina Mkoani Ruvuma lakini tunachokosea ni kuangalia mavazi yanayolingana na ngoma hiyo. Kwa mfano wangoni wana ngoma iitwayo Kitoto. Ngoma hii hutakiwa kuvaa vikokwa au Makokwa ya Mbegu za Embe. Pia vazi huwa rasmi kwa ngoma hiyo. Vazi la Kitoto lina kuwa la Asili kama Mavazi ya wamasai.
Hebu ona kila mmoja akiona Sikukuu au Maadhimisho ya Sherehe kama siku ya Maziwa, Ukimwi au Malaria hutoa Tshirt za Siku hiyo badala ya kuwaona wenye ngoma ili wajue Siku hiyo wangependa vazi gani. Hivi kazi ya Afisa Utamaduni ni nini. Hebu tuige mfano wa Alaiki ya Taifa tuone Maandalizi yanavyofanywa. WATANZANIA TUWE MACHO KULINDA UTAMADUNI WETU.

Monday, June 3, 2013

CCM MKOA WA RUVUMA WATAKIWA KUACHANA NA UBINAFSI KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI



Katibu mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani  Kinana  amewataka wana CCM kuacha tabia ya ubinafsi ambayo inaleta mfarakano ndani ya chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa chama Tawala cha CCM Taifa ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mabalozi wa manispaa ya songea wapatao 4297 semina iliyo fanyika uwanja wa majimaji songea.



Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM  Taifa Emanuel John Nchimbi amewataka wana CCM kuwa na Tahadhari na watu wanaotaka kuigawa Nchi kwa kutumia Ukabila au Dini akitoa Mfano wa Meseji zinazosambazwa amesema, "kuanzia jiwe la  mzungu hadi kilwa mto msimbati  mpaka ulipo ishia mto Ruvuma hadi bahari ya hindi ina faa kuitwa Tanzania ya kusini, mbona wenzetu Sudani  wamefanikiwa kujitenga mwisho wa kunukuu". Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Emanuel John Nchimbi amewaomba wana CCM kuji epusha na uchochezi huo;



Katibu mkuu wa CCM Taifa Abduramani Kinana amesema CCM imegundua kuwa chama cha mapinduzi kina pendwa na watu wengi  isipo kuwa baadhi ya watu katika chama  hupandikiza watu wasio kubalika ndiyo maana jimbo la songea lili weza kupoteza viti 6 vya Udiwani. Katibu mkuu wa CCM Abdurahamani Kinana amewataka wana CCM kuachana na tabia za ubinafsi kuchagua  kwa kusema huyu ni mwenzetu mtindo huo uachwe mara moja

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Ruvuma akitoa Tarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani Kinana katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma
Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika uwanja wa Majimaji wakati wa semina kwa Mabalozi wa CCM Manspaa ya Songea


Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimepoteza Viti zaidi ya 6 kwa sababu ya Ubinafsi kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja kuliko kujali Maslahi ya Watu wengi na walio wengi kusema bora tupoteze  ili tukose Wote

Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akionyesha alivyo fufuka na chama cha Mapinduzi katika onyesho maalum kwa Katibu mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdurahamani Kinana
Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akiwa ndani ya Jeneza katika uwanja wa Majimaji Songea huku moto ukiunguza jeneza hilo lakini alipo fufuka akatoa kauli amefufuka na Chama Cha Mapinduzi