Katibu mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani Kinana
amewataka wana CCM kuacha tabia ya ubinafsi ambayo inaleta mfarakano
ndani ya chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa chama Tawala cha CCM Taifa ameyasema
hayo wakati akifungua semina ya mabalozi wa manispaa ya songea wapatao 4297
semina iliyo fanyika uwanja wa majimaji songea.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Emanuel John Nchimbi amewataka wana CCM
kuwa na Tahadhari na watu wanaotaka kuigawa Nchi kwa kutumia Ukabila au Dini
akitoa Mfano wa Meseji zinazosambazwa amesema, "kuanzia jiwe la mzungu hadi kilwa mto msimbati mpaka ulipo ishia mto Ruvuma hadi bahari ya hindi ina faa
kuitwa Tanzania
ya kusini, mbona wenzetu Sudani
wamefanikiwa kujitenga mwisho wa kunukuu". Mjumbe wa kamati kuu
ya CCM Emanuel John Nchimbi amewaomba wana CCM kuji epusha na uchochezi huo;
Katibu mkuu wa CCM Taifa Abduramani Kinana amesema CCM
imegundua kuwa chama cha mapinduzi kina pendwa na watu wengi isipo kuwa baadhi ya watu katika chama hupandikiza watu wasio kubalika ndiyo maana
jimbo la songea lili weza kupoteza viti 6 vya Udiwani. Katibu mkuu wa CCM Abdurahamani
Kinana amewataka wana CCM kuachana na tabia za ubinafsi kuchagua kwa kusema huyu ni mwenzetu mtindo huo uachwe
mara moja
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma akitoa Tarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdurahamani Kinana katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma
Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika uwanja wa Majimaji wakati wa semina kwa Mabalozi wa CCM Manspaa ya Songea
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimepoteza Viti zaidi ya 6 kwa sababu ya Ubinafsi
kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja kuliko kujali Maslahi ya Watu wengi na
walio wengi kusema bora tupoteze ili
tukose Wote
Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akionyesha alivyo fufuka na chama cha Mapinduzi katika onyesho maalum kwa Katibu mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdurahamani Kinana
Msanii wa Kikundi cha Maiko Jacksoni akiwa ndani ya Jeneza katika uwanja wa Majimaji Songea huku moto ukiunguza jeneza hilo lakini alipo fufuka akatoa kauli amefufuka na Chama Cha Mapinduzi
No comments:
Post a Comment