Hivi karibuni nilizungumzia kuhusu kupotea kwa lugha ya Asili kwa karine chache zijazo. Hebu sasa nizungumze kuhusu Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma. Hasa kuhusu Utamaduni wetu.
Tuna Ngoma za kila aina Mkoani Ruvuma lakini tunachokosea ni kuangalia mavazi yanayolingana na ngoma hiyo. Kwa mfano wangoni wana ngoma iitwayo Kitoto. Ngoma hii hutakiwa kuvaa vikokwa au Makokwa ya Mbegu za Embe. Pia vazi huwa rasmi kwa ngoma hiyo. Vazi la Kitoto lina kuwa la Asili kama Mavazi ya wamasai.
Hebu ona kila mmoja akiona Sikukuu au Maadhimisho ya Sherehe kama siku ya Maziwa, Ukimwi au Malaria hutoa Tshirt za Siku hiyo badala ya kuwaona wenye ngoma ili wajue Siku hiyo wangependa vazi gani. Hivi kazi ya Afisa Utamaduni ni nini. Hebu tuige mfano wa Alaiki ya Taifa tuone Maandalizi yanavyofanywa. WATANZANIA TUWE MACHO KULINDA UTAMADUNI WETU.
Ombi :-mimi ni mkereketwa sana wa uasili je ubaweza kurekodi pia?. i
ReplyDelete