Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
Viongozi wandamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali la RUNECISO wakielekea Katika Jiwe la Pomonda kuona hali ya Pamgo lilipo katika Jiwe hilo ambalo lilihifadhi watu waliojificha wakati wa Vita vya 1 na vya 2 vya Dunia
Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
Katibu Muhtasi wa RUNECISO akiwa katika utalii nyuma ya Jiwe hilo la Pomonda eneo la Ziwa Nyasa akichukua kumbukumbu za Historia ya eneo hilo na Mabadiliko yaliyopo pembeni kushoto kwake ni mti ambao una umri zaidi ya karne moja lakini haukui zaidi ya hapo.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Viongozi waandamizi wa RUNECISO hapo wakiwa ndani ya Jiwe hilo la kihistoria na kivutio cha watalii, picha unayoiona ni ndani ya pango la Pomonda ambalo lina uwezo wa kuhifadhi watu zaidi ya 250 kwa wakati mmoja lililotumiwa kujificha wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambapo wazalendo wa Kitanzania walikuwa wanajificha. Aliyekaa Chini ni Makamu Mwenyekiti wa RUNECISO na Mwandishi wa Star Tv akiwa amechoka baada ya kupanda kwa shida jiwe hilo hadi kulifikia Pango.
Hizi ni Nyumba zilizopo katika ufukwe wa Ziwa Nyasa za wakazi wa kawaida wanaofaidi Ufukwe wa Ziwa Nyasa.
No comments:
Post a Comment