Mhandisi Vinisent Njila amesema ametoa Msaada huo yeye na
mwenzie Joseph Londo wa Jezi za Kike na za kiume pamoja na Mipira miwili wa
kike na wa kiume vyote vikiwa na thamani ya Shilingi laki nne (400,000) ikiwa
ni moja ya shukrani ya shule hiyo kwa kumpa msingi wa maisha
Mama mzazi wa Mhandisi Vinsent Njila akielza alivyo pata Tabu katika kumsomesha Mtoto wake lakini amesema Mvumilivu hula Mbivu, Ukiwekeza katika elimu omba Mungu mtoto wako awe kichwa utafaidi amesema mama Mhandisi
Mhadisi wa Umwagiliaji wa Nyanda za Juu Kusini kwa Mikoa ya
Lindi, Mtwara na Ruvuma amewaomba wasomio
mbalimbali kukumbuka walikotoka kwa kutoa Misaada katika Shule walizosoma.
Mhandisi wa Umwagiliaji Nyanda za Juu Kusini Vicenti Njila
ameyasema hayo wakati akitoa Msaada wa Vifaa vya Michezo katika Shule ya Msingi
Chiulu aliyosoma mwaka 1970 na kumfanya awe Mhandisi baada ya kumaliza Shule
hiyo.
Mhandisi Vinisent Njila amesema ametoa Msaada huo yeye na
mwenzie Joseph Londo wa Jezi za Kike na za kiume pamoja na Mipira miwili wa
kike na wa kiume vyote vikiwa na thamani ya Shilingi laki nne (400,000) ikiwa
ni moja ya shukrani ya shule hiyo kwa kumpa msingi.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi Chiulu Mwalimu amesema anashukuru kwa kupata msaada wa
Jezi na Mipira hiyo itakuwa chachu ya kuwafanya Wanafunzi wasome kwa bidii ili
na wao siku zijazo waweze kutoa Msaada kwa wenzao.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Chiulu katika wilaya ya Nyasa akipokea jenzi kwa ajili ya shule hiyo kutoka kwa Vinsent Njila
Mhandisi wa Nyanda za juu kusini Vinsent Njila akikabidhi Mpira wa Miguu kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Chiulu wilayani Nyasa
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chiulu akipokie zawadi ya jezi za kiume kutoka kwa Mhandisi Vinsent Njila
Mhandisi Vinisent Njila Amesema inatia aibu kuona wasomi waliosoma Shuleni hapo
wakiwa na Maendeleo lakini hawakumbuki walikotoka, hizo ndizo sababu
zilizotusukuma kutoa zawadi hizo katika Shule ya Msingi Chiulu
Baba Mzazi wa Vinsent Njila akieleza changamoto za kusomesha mwanafunzi amesema kusomsha kuna taka moyo hasa kwa sisi tunao ishi pembezoni ambako hakuna miundo mbinu ya biashara, kinacho takiwa ni imani tu, Ndivyo nilivyo fanikiwa kumsomesha Vinsent Njila, Jambo kubwa ni kuepuka na makundi yasiyo jali elimu alimaliza
Ukifika katika Wilaya ya Nyasa Kitoweo kikubwa ni Samaki , hao unao waona ni samaki aina ya Mbufu ambao ni watamu kupita samaki ulio wahi kula
No comments:
Post a Comment