LUKONDONYIKA NAVACHE wawanawake walio olewa na wapare wanao ishi mkoa wa Ruvuma wameguswa na watoto yatima ambao wanaishi kituo cha chipole kinacho milikiwa na watawa wa kikatoriki songea vijijini waliweza kupeleka misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kama wanavyo onekana hapo juu
sisita Akwinata akiwa Chipole akipokea msaada wa zawadi mbambali kutoka kwa Chama cha wanawake wakipare walio olewa Mkoa wa Ruvuma
Mama wa Kipare akiwa amempakata mtoto mdogo aliye telekezwa na mama yake na kupelekwa kituo cha kulelea watoto wadogo kilichopo Chipole Songea vijijini
Mama wa Kipare ambaye pia ni mfanyakazi wa Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma akiwa ameguswa na watoto Yatima walioko Chipole Songea Vijijin alikuwa mmoja wawanawake wakipare walio kwenda kutoa zawadi kwa watoto yatima Mungu awaongezee pale walipo chukua
Ukiwa mama ,Sifa ya kwanza ya Mama ni kuwa na Huruma wanawake wakipare wanao ishi mkoani Ruvuma w Chipoleameonyesha Huruma hiyo kwa kwenda kutoa zawadi na kuwa fariji watoto wanao ishi katika mazingira magumu kwa kutegemea nguvu za masister wa
Hata ukiwa umetingwa kiasi gani lakini unapo kutana na mtoto mdogo moyo wako huwa na furaha kupita kiasi kama unavyo mwona mama huyu hapo juu akiwa amemshika mtotot yatima,jee wewe unaye soma habari hii umewahi kutoa msaada kwa watoto yatima ,unangoja kulizwa na malaika au Mungu ?
Hawo wote unao waona hapo ni watoto ambao hawana baba wala mama wana hitaji msaada wako ni kweli una lala usingizi mzuri huku watoto kama hao wakiwa katika huzuni ya kukosa wazazi na vyakula ,mavazi,pamoja na kutaka kufarijiwa
Hebu angalia watoto wanavyo furahia zawadi hata ikiwa nikidogo wanacho furahia watoto hawa ni upendo wako wewe na mimi
Hebu angalia Mtoto huyu ana hitaji upendo lakini ni Yatima ana taka kuwa karibu na jamii jee wewe hili halikugusi mpaka waje wanawake wakipare na hapa Ruvuma kuna watu,ni vizuri fedha yako kuitumia kwenye pombe,anasa zisizo na faida ?
watoto hawa walipo tembelewa na Wanawake wa Kipare walifarijika sana hapo wanawake hao wakitoa mipira kwa ajili ya kuchezea hao watoto
Mtoto amepakwatwa huku akiwa ameshika maziwa ya maji ,huo ni upendo wa akina mama wa kipare wanao ishi Mkoani Ruvuma
Watoto wakinywa maziwa na wakionyesha furaha kwa wageni wao ndugu yangu na kukumbusha kazi hiui na wewe tafadhali ifanye Mungu ata kuongezea
Watawa wa kike wa Kanisa katolick Chipole wakionyesha jinsi wanavyo wajali watoto wana tupwa na akina mama wasio na huruma
Watoto hawa yatima wakisha kua hufanya kazi ambazo zina weza kuwaletea chakula hapo wapo katika busitani wakilima
Moyo wakufariji Yatima una tegemea na wewe ulivyo lelewa ukiwa Binadamu utafanya anayo fanya mama huyo pichani lakini kuwa hujalelewa uta baki kwenye anasa tu
Watoto hao hapo juu ni baadhi ya Mayatima kwa ujumula wao wapo mayatima 60 ambao wana hitaji msaada jipime wewe kwanza una mtoto mmoja nyumbani kwako jee hali inakuwaje kibajeti ukipata jibu basi toa msaada kwa watoto hawa
Akina Mama hawa Wakipare wanahitaji Pongezi kwa kazi kubwa waliyo ifanya watoto hawa Yatima wapatao 60 kwa zawadi hizi zizapunguza maumivu ingawa siyo sana, uliye baki kutoa msaada ni wewe na mimi ingawa mimi nime fikisha ujumbe hiyo haitoshi
Mwenye Macho haambiwi ona bali hutumia Macho yake unaona umati wa watoto ulivyouna ngoja Huruma ya Jamii jisifu umetoa sadaka kwa watoto kama hawa, Nasiyo kusema na tika kula sadaka ya Marehemu fulani iko siku sadaka hiyo itakutokea puani
KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo
UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Sunday, June 22, 2014
Saturday, June 21, 2014
KWA NINI WATU HAWAACHI VITENDO VYA USHIRIKINA ,WAONE WACHAWI WA SONGEA MKOANI RUVUMA
Umewahi kuona kibuyu kikizunguza basi ukipata nafasi ukikutana na Mzee Alex Haule atakueleza kwa kirefu, unakiona kibuyu hicho alicho kamata hapo hana ujanja wa kishirikina kila kitu ana sema mwenyewe
Mzee Alex Haule akiwa amekaa Uwanja wa Zambi na Mganga wa Jadi Binti ndembo akieleza jinsi alivyo ua Watoto wake wa NNE kwa njia ya Ushirikina aliye kulia ni Mzee mshirikina Beda Nchimbi liye vaa shati jeupe ,Hivyo vipara vina maana yake fika uwanja wa zambi uta jua maana ya upara
Mzee Beda Nchimbi kutoka Parango Peramiho Songea Vijijini aliye vaa Shati Jeupe amambaye ameua wajukuu wanne akiwa uwanja wa Zambi akitubu Matendo maovu aliyo yafanya kwa Jamii
Bint Ndembo akiwa na kioo cha ajabu ambacho huangalia matendo mabovu yanayo tendwa na washirikina
Washirikina wakivua viatu mara wanapo ingia uwanja wa Zambi tayari kwa kuumbuliwa Maovu yao
Ukiangalia kwa Makini hapo wanapo kaa hao watu kuna duara la rangi nyeupa kwa hapo chini ukikalia duara hilo basi wewe kama Mshirikina utaeleza kila kitu ulicho kuwa nacho hata dawa unazo tumia uta eleza :Unachezea Bint Ndembo wewe:
Kutoka kulia ni Mzee Alex Haule ambaye ameua watoto wake wa Nne kwa ajili ya Sikukuu mbalimbali. wa kwanza kushoto ni mzee Beda Nchimbi ambaye naye ameua wajukuu wake Nne kwa ajili ya Kitoweo kama alivyo dai mwenyewe,
Monday, June 16, 2014
WATOTO WA MANSPAA YA SONGEA WAOMBA ULINZI KWA VITENDO VYA UBAKAJI
Wafanyakakazi waCRDB wakiwa katika siku ya Mtotot wa Afirica huku wakifanya kazi
kuweka akiba kwa watoto ni mhimu fungua akaunt ya Junior Jumbo imusaidie mtoto wako badaye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ameyasema hayo wakati wa
Maazimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Majengo Manispaa ya Songea
Mstaiki meya amekea adhabu ngumu wanazo pewa watoto kuwa choma
moto,kuwafanyisha kazi ngumu pamoja na matendo mabaya ya kuwa baka watoto
wakike.
watoto wanahitaji ulinzi wanapo kuwa wana rudi shuleni wewe na mimi ni walinzi wawatoto |
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la
Songea Enock Lugenge amewataka Wazazi kufungua Akaunzi ya Junior Jumbo ili
kuweza kumwekea Mtoto Akiba kwa ajili ya Masomo, Afya na Akiba ya baadaye,
Benki ya CRDB Tawila la Songea katika Kuazimisha Siku ya Mtoto wa Afrika
wametoa zawadi za Daftari, peni na sare za Mtoto wa Afrika kwa Watoto zaidi ya
100 waliohudhuria Sherehe za Mtoto wa Afrika.
Saturday, June 14, 2014
WAZEE WAOMBA KUPATA MBUNGE MWAKILISHI WA KUWAKILISHA WAZEE
Mtendaji wa Kata ya Matogoro akitoa neno la utangulizi kuwa karibisha wazee katika ofisi yake Matogoro Manispaa ya Songea
Mkusanyiko wa wazee wapatao 500 waliokuja kuishindikiza Serekari kuwapa mwakilishi Bungeni
Wazee wa Mnspaa ya Songea Wapatao 500 wakiwa viwanja vya Matogoro wakitoa sababu za kutaka kuwa na mwakilishi Bungeni wamedai ni kutokana na kuto sikilizwa kero zao
Afisa Maendeleo Manspaa ya Songea Adam Ngelangela akijibu baadhi ya kero zilizo telewa na wazee na kusema ziko kero nyingi zilizo tatuliwa ikiwa na pomoja na wazee kutibiwa bure
Wazee wakitia sahihi karatasi linalo onyesha wao wanataka kuwa na mwakilishi Bungeni
Mwenyekiti wawazee Manspaa ya SongeaAhamad Mwamba akiwahutubia wazee wenzake jinsi wanavyo kosa haki za msingi wanapo kosa kuwa na mwakilishi Bungeni ambaye atachaguliuwa kutokana na Wazee
MWENYEKITI WA WAZAZZI TAIFA A WATUHUMIWA WAZAZI WA KIKE KUWAPOTOSHA MAADILI YA WATOTO WA KIKE
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo amesema
kuharibika kwa Tabia za Watoto kwa Kiasi Kikubwa kunasababishwa na Wazazi wa Kike, Mtoto anapokuwa anabadilika
kitabia na kumiliki Vitu vya Anasa na vyenye thamani ya juu kuliko uwezo wa
wazazi ni juu yao kuhoji ili kujua Mtoto wao amevipata wapi.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo
akiwa Mkoani Ruvuma amezitaka Halmashauri za
wilaya na manspaa ya mji kutoa Asilimia 10% zilizotengwa na Serikali kwa
ajili ya kuwasaidia Vijana na Wanawake kuwainua
kiuchumi.
Wazazi waliohudhuria katika Mkutano Kijijini Matetereka wametoa
kero zinazowakabili ikiwemo, Watendaji wa Serikali kuwa Miungu watu, Walemavu
kukosa Msaada kutoka kwa Viongozi wao, na kwa upande wa Wazazi wa Kike
wakijitetetea wamesema Utandawazi ndiyo sababu kubwa inayowafanya
watoto wao kuharibika.
Mheshimiwa Diwani Teofilo Mlelwa akimkaribisha mwenyekiti wa Taifa wawazazi Alhaji Abdallah Majura Bulembo katika kata ya MkongotemaWanafunzi wa Shule ya Wilima wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Viongozi wa CCM Songea vijijini walio shiriki ziara ya Mwenyekiti wa Wazazi taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Wazee wakiwa katika mkutano wawazazi katika kijiji Mkongotema songea vijijini
Wazee wa Wilima wakisikiliza hotuba ya Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi CCM Taifa Alhaji Abdallah
Majura Bulembo amewaasa Wazazi kuacha Tabia ya kusababisha Watoto wa kike kuharibika kitabia hatimaye kupata uja uzito .
Mwenyekiti wa Jumuya ya Wazazi Taifa Alhaji Abdallah
Majura Bulembo ameyasema hayo akiwa katika Kijiji cha Matetereka Kata ya
Gumbiro Songea Vijijini Wakati wa Ziara yake Mkoani Ruvuma.
katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma akimpokea Mwenyekiti taifa Alhaji Abdallah Majura BulemboDiwani TT wapili akiwa na furaha baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wawazazi TaifaAlhaji Abdallah Majura Bulembo
Mlemavu wa viungo akiwa katika mkutano wa mwenyekiti wa wazazi Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulemboakiomba msaada wa Baiskeli |
Subscribe to:
Posts (Atom)