Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti
amewataka Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuepukana na Rushwa, pamoja na kuepuka
Tamaa ambayo inaifanya Nchi kuporomoka kimaendeleo
..
Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti
ameyasema hayo katika Semina ya Upimaji wa Afya za Watumishi wa Idara ya
Uhamiaji na Familia zao.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiri tayari kwa kushiriki upimaji wa hiari wa virusi vya ukimwi
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza amesema
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameisaidia Idara yake kuwavumbua wahamioaji Haramu,
jambo ambalo limepunguza kuingia kwa Wahamiaji Haramu kutoka 200 hadi sasa
imekuwa ndoto.
Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wakisikiliza kwa makini jinsi ya kuepukana na maambukizi ya VVU na UKIMWI mjini SongeaMaandamano ya kuhamasisha familia ya Uhamiaji Mkoani Ruvuma kupima kwa hiari ili kujua Afya zao pichani Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti katikati na kushoto kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza
Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kushoto George Chiposi akiwa na Afisa Usama Mkoa wa Ruvuma kulia
Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu , amesema Idara ya Uhamiaji ni tigemeo la Taifa la Tanzania, kwani wao ndio wanaounganisha mahusiano mazuri na Nchi nyingine, kuepuka Masuala ya Rushwa ni njia moja wapo ya kutangaza Uadilifu wa Watanzania. Ni juu ya Idara ya Uhamiaji kuepuka Tamaa zinazoweza kuondoa heshima ya taifa la Tanzania.
Maandamano ya upimaji wa Hiari ya kiingia katika Viwanja vya Angoni katika Manspaa ya Songea
Familia za Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma wakishiriki semina ya upimaji wa hiari wa VVU na UKIMWI Mkoani Ruvuma
Familia ya wafanyakazi wa idara ya Uhamiaji wakliwa katika semina ya upimaji wa hiari kuhusu Afya zao
Afisa uhamiji Shabani akiongoza Maandamano kutoka jengo la Uhamiaji hadi uwanja wa Angoni Songea
Nao akinamama walio kuja kushiriki upimaji wa hiari kwa
watumishi wa idara ya uhamiaji wameomba zoezi la hilo lifike hadi kwa watoto wa
familia ya uhamiaji.
Siku ya Upimaji wa Afya ya Wafanya Kazi wa Idara ya
Uhamiaji ililenga kujua Magonjwa ya Saratani, Maambukizi
ya VVU/UKIMWI na Presha.
Afisa Usalama Mkoa wa Ruvuma Akisikiliza kwa makani Mada za kuepukana UKIMWI na VVU
No comments:
Post a Comment