KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, June 16, 2014

WATOTO WA MANSPAA YA SONGEA WAOMBA ULINZI KWA VITENDO VYA UBAKAJI



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama amewataka Wazazi kutoa Malezi mema kwa Watoto, kuanzia Malazi, Mavazi, Chakula na Elimu ili Watoto wakue katika Afya nzuri.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea amesema kuharibika kwa tabia za Watoto kunatokana na Watoto kukosa Malezi mema kutoka kwa Wazazi.
Wazazi waliohudhuria Sherehe hizo wakiwakilishwa na Judith Lugoye wameiomba Serikali kuwa na Silabasi zisizobadilika mara kwa mara katika masomo ili kuweza kumpa ufahamu Mtoto wa kuelewa Masomo anayofundishwa. Pia wameomba adhabu za viboko zitolewe kulingana na umri Fimbo anayopigwa mtoto wa darasa la kwanza itofautiane na anayopigwa wa darasa la saba

 Wafanyakakazi waCRDB wakiwa katika siku ya Mtotot wa Afirica huku wakifanya kazi
kuweka akiba kwa watoto ni mhimu fungua akaunt ya Junior Jumbo imusaidie mtoto wako badaye

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ameyasema hayo wakati wa Maazimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Majengo Manispaa ya Songea Mstaiki meya amekea adhabu ngumu wanazo pewa watoto kuwa choma moto,kuwafanyisha kazi ngumu pamoja na matendo mabaya ya kuwa baka watoto wakike.
watoto wanahitaji ulinzi wanapo kuwa wana rudi shuleni wewe na mimi ni walinzi wawatoto

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Songea Enock Lugenge amewataka Wazazi kufungua Akaunzi ya Junior Jumbo ili kuweza kumwekea Mtoto Akiba kwa ajili ya Masomo, Afya na Akiba ya baadaye, Benki ya CRDB Tawila la Songea katika Kuazimisha Siku ya Mtoto wa Afrika wametoa zawadi za Daftari, peni na sare za Mtoto wa Afrika kwa Watoto zaidi ya 100 waliohudhuria Sherehe za Mtoto wa Afrika.

No comments:

Post a Comment