LUKONDONYIKA NAVACHE wawanawake walio olewa na wapare wanao ishi mkoa wa Ruvuma wameguswa na watoto yatima ambao wanaishi kituo cha chipole kinacho milikiwa na watawa wa kikatoriki songea vijijini waliweza kupeleka misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kama wanavyo onekana hapo juu
sisita Akwinata akiwa Chipole akipokea msaada wa zawadi mbambali kutoka kwa Chama cha wanawake wakipare walio olewa Mkoa wa Ruvuma
Mama wa Kipare akiwa amempakata mtoto mdogo aliye telekezwa na mama yake na kupelekwa kituo cha kulelea watoto wadogo kilichopo Chipole Songea vijijini
Mama wa Kipare ambaye pia ni mfanyakazi wa Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma akiwa ameguswa na watoto Yatima walioko Chipole Songea Vijijin alikuwa mmoja wawanawake wakipare walio kwenda kutoa zawadi kwa watoto yatima Mungu awaongezee pale walipo chukua
Ukiwa mama ,Sifa ya kwanza ya Mama ni kuwa na Huruma wanawake wakipare wanao ishi mkoani Ruvuma w Chipoleameonyesha Huruma hiyo kwa kwenda kutoa zawadi na kuwa fariji watoto wanao ishi katika mazingira magumu kwa kutegemea nguvu za masister wa
Hata ukiwa umetingwa kiasi gani lakini unapo kutana na mtoto mdogo moyo wako huwa na furaha kupita kiasi kama unavyo mwona mama huyu hapo juu akiwa amemshika mtotot yatima,jee wewe unaye soma habari hii umewahi kutoa msaada kwa watoto yatima ,unangoja kulizwa na malaika au Mungu ?
Hawo wote unao waona hapo ni watoto ambao hawana baba wala mama wana hitaji msaada wako ni kweli una lala usingizi mzuri huku watoto kama hao wakiwa katika huzuni ya kukosa wazazi na vyakula ,mavazi,pamoja na kutaka kufarijiwa
Hebu angalia watoto wanavyo furahia zawadi hata ikiwa nikidogo wanacho furahia watoto hawa ni upendo wako wewe na mimi
Hebu angalia Mtoto huyu ana hitaji upendo lakini ni Yatima ana taka kuwa karibu na jamii jee wewe hili halikugusi mpaka waje wanawake wakipare na hapa Ruvuma kuna watu,ni vizuri fedha yako kuitumia kwenye pombe,anasa zisizo na faida ?
watoto hawa walipo tembelewa na Wanawake wa Kipare walifarijika sana hapo wanawake hao wakitoa mipira kwa ajili ya kuchezea hao watoto
Mtoto amepakwatwa huku akiwa ameshika maziwa ya maji ,huo ni upendo wa akina mama wa kipare wanao ishi Mkoani Ruvuma
Watoto wakinywa maziwa na wakionyesha furaha kwa wageni wao ndugu yangu na kukumbusha kazi hiui na wewe tafadhali ifanye Mungu ata kuongezea
Watawa wa kike wa Kanisa katolick Chipole wakionyesha jinsi wanavyo wajali watoto wana tupwa na akina mama wasio na huruma
Watoto hawa yatima wakisha kua hufanya kazi ambazo zina weza kuwaletea chakula hapo wapo katika busitani wakilima
Moyo wakufariji Yatima una tegemea na wewe ulivyo lelewa ukiwa Binadamu utafanya anayo fanya mama huyo pichani lakini kuwa hujalelewa uta baki kwenye anasa tu
Watoto hao hapo juu ni baadhi ya Mayatima kwa ujumula wao wapo mayatima 60 ambao wana hitaji msaada jipime wewe kwanza una mtoto mmoja nyumbani kwako jee hali inakuwaje kibajeti ukipata jibu basi toa msaada kwa watoto hawa
Akina Mama hawa Wakipare wanahitaji Pongezi kwa kazi kubwa waliyo ifanya watoto hawa Yatima wapatao 60 kwa zawadi hizi zizapunguza maumivu ingawa siyo sana, uliye baki kutoa msaada ni wewe na mimi ingawa mimi nime fikisha ujumbe hiyo haitoshi
Mwenye Macho haambiwi ona bali hutumia Macho yake unaona umati wa watoto ulivyouna ngoja Huruma ya Jamii jisifu umetoa sadaka kwa watoto kama hawa, Nasiyo kusema na tika kula sadaka ya Marehemu fulani iko siku sadaka hiyo itakutokea puani
No comments:
Post a Comment