Watoto wa Marehemu Captn John Damian komba Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mangharibi wakiwa katika foleni ya kwenda kuweka Mavumbi katika Kaburi la baba yao mpendwa ikiwa ni Ishara ya kumbukumbu ya kuwa mwanadamu yu mavumbi katika Imani ya Kikristu.
Wafanya Kazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioongoza kubeba Jeneza la la Marehemu Captn John Komba wakiwa katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji ambako shughuli ya kuaga mwili wa Captn Komba ilifanyika mara baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akifanya Mawasiliano ya namna ya kufanikisha Mazishi ya Marehemu Captn John Damian Komba Kijijini kwake Lituhi Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma
Waombolezaji mbalimbali wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma waliojitokeza kuupokea mwili wa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mangharibi Marehemu Captn John Damian Komba katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwa katika Viwanja vya Maombolezo Lituhi Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma ambako Mazishi ya Captn Komba yalifanyika. Kutoka kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mh, Mwanahamis Kwariko, anayefuatia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anna Makinda, anafuatia Waziri Mkuu Mstaafu Edward lowasa na wanaofuata ni Familia ya Marehemu Captn Komba.
Hapo Makaburi ya Lituhi ambapo jeneza lililowekwa Mwili wa Marehemu Captn John Komba likishuswa katika Makazi ya Milele, Walioshika jeneza ni Wabunge na wafanyakazi wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Anna S. Makinda akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
|
Naye Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda amesema Binadamu hivi sasa
wanajiingiza katika Vitendo viovu kuliko kukimbilia Amani, ni juu ya Watanzania
kuaca Tabia ya
Naibu Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Joel akielezezea namna kilivotokea Kifo cha Captn john Damian Komba baada ya kuwasili katika Uwanja wa majimaji ambako wananchi walijitokeza kuupokea na kuuaga mwili wa Marehemu Captn John komba.
Rais wa Malawi Bakili Mluzi alitoa salamu
za rambirambi kwa serekari ya Jamuhuri ya Tanzani kupitia kwa mbunge dr emanuel mchimbi salamu
zilizo somwa na Afisa wa Bunge Yakubu Yakubu amesema amesitushwa na kifo cha
cap john komba anamwomba mungu amweke mahali pema peponi
|
|
Serikai ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kusimamia Miradi
yoye iiyoahidiwa na Marehemu Captn John Damian ambayo tayari ilishaingizwa
katika Sera ya Chama cha Mapinduzi.Mheshimiwa Jenista Mhagama ameyasema hayo wakati
akitoa Salamu za Serikai za Rambirambi kwa familia ya Marehemu Captn
John Damian Komba na kwa Watanzania kwa
ujumla
|
Mh. Jenista Mhagama amesema
Serikali imepata Pengo kubwa kutokana na kifo cha cap John Komba kwa juhudi na kazi ailizokuwa akizifanya za kuleta maendeleo , amesema Serikali
inathamini mchango mkubwa uliotolewa na Capt John Komba, Kwa hiyo Wananchi wa
Jimbo a Mbinga Mangharibi wajue Maendelo yapo pale pale walichokikosa ni
kutoweka kwa Marehemu Captn John Komba.
Katapila iliyotumika kubeba mfuniko wa Kaburi wenye uzito wa Tani Tatu ikiwa Jirani na kaburi tayari kwa kuinua Funiko hilo baada ya Jeneza Kushushwa Kaburini.
Mhashamu Askofu John komba akibariki Jeneza la Marehemu Captn Komba katika Ibada ya kumwombea iliyofanyika katika Uwanja wa Michezo wa lituhi Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
Hapo wafanyakazi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania na Kamati ya Mazishi ya Mkoa wa Ruvuma wakiinua Jeneza baada ya Ibada kumalizika tayari kwa kuelekea Makaburini kwa Mazishi.
Zaidi ya watu 20, wakiwa wameshika jeneza kwa makini lililobeba Mwili wa Marehemu Captn John Komba tayari kwa kulishusha kaburini katika Makao ya milele katika Makaburi ya lituhi Nyasa Mkoani Ruvuma.
Jeneza la Captn John Komba likiwa juu ya Kaburi kabla ya kulishusha kaburini.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Lituhi waliokuwa wamepanda juu ya miti ili kushuhudia kinachoendelea katika Mazishi ya Mbunge wao wa Jimbo la mbinga Mangharibi kutokana na umati wa watu waliokuwa wamfurika kuja kumzika Captn John Damian Komba.
Hapo Ibada ya kumuombea Marehemu Captn John Komba ikiwa inaendelea katika Uwanja wa Lituhi kijijini kwake Marehemu muda mfupi kabla ya Mazishi.
Askofu wa jimbo la Mbinga Mhashamu Askofu John Komba akisoma Misa ya mazishi ya Kumuombea Marehemu Captn John Komba Lituhi Wilayani Nyasa. Waliosimama jirani na Jeneza ni Wafanya kazi wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa tanzania ambao ndio walikuwa wanlibeba Jeneza la Captn Komba.
Katika hali isiyo ya kawaida Cap
John Komba Alishachora ramani ya kaburi lake na alishatengeneza mlango wa zege wenye uzito wa Tani 3 ambao uliwekwa na Kijiko
cha katapira
Hapo Jeneza likishushwa kwenye Ndege, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akipokea Jeneza la Mwili wa Marehemu Captn John Damian Komba ulipowasili Mkoani kwake katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mh. dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali katika viwanja vya Makaburi ya lituhi ambako Mazishi ya Captn John Komba yalifanyika
Kutoka kushoto Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akifuatia na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma kikwete wakiwa katika Mazishi ya Captn John Komba Kijijini Lituhi Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
|
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akipokea Taji la Shada la Maua ili akaweke juu ya kaburi la Captn John Komba. |
Mazishi ya Marehemu Captn John Damian Komba yaliongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Misa Takatifu ya kumwombea Captn john Komba iliongozwa na
Askofu Johhn Komba wa Jimbo la Mbinga,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka Mavumbi katika Kaburi la Marehemu Captn John Komba.
Viongozi wengine
waliohudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa.
Naibu waziri wa fedha Mwigulu Lameki Nchemba,
waziri wa Kilimo chakula na
Ushirika Steven Wasira,Viongozi wa chama waliongozwa na katibu mkuu wa CCM
taifa Abrahmani kinana