Mkuu wa Majeshi
Nchini Tanzania amewataka Watanzania kuwa na kitu cha kujivunia baada ya Maisha
haya ya Dunia.
Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania General Venance Mabeyo ameyasema hayo katika
kumbukizi ya Mashujaa wa vita vya Majimaji iliyofanyika katika uwanja wa
Mashujaa Mahenge, Mkuu wa Majeshi amesema tunapowakumbuka Mashujaa ni lazima
tujue sisi tumefanya nini kwa Taifa letu lazima tujitoe kulinda Taifa letu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaomba Wananchi na Jeshi la Wananchi Tanzania kuendelea kulinda Raia na kuendeleza Amani iliyopo Tanzania
Chifu wa wangoni chifu Emanuel Zulu akishirikiana na Mzee wa Baraza la
Machifu Yasini Mbano am muomba Mkuu wa Majeshi ili kuongeza Amani katika Mioyo
wana Ruvuma wameomba Rais Magufuli
atembelee Mkoa wa Ruvuma.
Mzee wa Baraza la Wazee kutoka Matimila Yasini Mbano akiwa akifuatiwa na Chifu Emanuel Zuru anaye fuatia Mkuu waMajeshi Nchini Jenelali Venance Mabeyo na wa Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Cristine Mndeme
Mzee Yasini Mbano akitoka kuweka Rungu kwenye Mnara wa kumbukumbu wa Vita vya Nduli Iddi Amini Dada wa Uganda
Pamoja na Tumbuizi za ngoma
ya Asili pia kulikuwepo na sanaa za Vijana wa JKT Mlale ambao waliwakumbusha
wananchi umuhimu wa kudumisha Amani tuliyonayo na kuwatii viongozi wetu tuliowachagua.
Kiongozi wa Dini ya Kristo akitoa Dua kwa kuwaombea Mashujaa walio kufa miaka 112 iliyo pita katika vita vya Majimaji
Mkuu wa Majshi Nchini Tanzania akiweka shahada la Maua kwa Mashujaa 66 walio zikwa kwenye kaburi moja katika viwanja vya mahenge Manspaa ya Songea
Mkuu wa Majeshi Nchini
Tanzania Jenerali Mabeyo amehaidi
kujenga Ukumbi wa Mikutano katika viwanja vya Makumbusho ya Majimaji vilivyopo
Mahenge manispaa ya Songea. Insert
Kutoka kulia Mzee wa Baraza la Wazee Yasini Mbano wapili kutoka kulia Chifu Emanuel Zulu na anaye fuatia ni Mkuu wa Majeshi Nchini Jenelali Venance Mabeyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Tanzania amesema Maombi ya
kujenga Ukumbi wa Makumbusho ya Majimaji Jeshi litajenga pia kila Mwaka Jeshi
litafanya Paredi ya kuwaenzi Mashujaa hao.
Emanuel Zuru Chifu wa Kingoni katikati Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo na Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Cristine Mndeme
Wageni waalikwa kutoka Malawi na Nchi jirani zinazopakana na
Mkoa wa Ruvuma wameshukuru uhusiano wa kitamaduni kualikwa katika sherehe hii
kubwa ya kukumbuka Mashujaa 66 walionyongwa wilayani Songea.
|
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Nchini Tanzani Jeneral
Venance Mabeyo amewataka watanzania kuenzi Mila na Utamaduni wa Mtanzania ambao unaonyesha ni njia moja wapo ya kuweza kuongeza Ajira kwa Vijana wa Taifa Tanzania.
Mkuu wa Majeshi Nchini
Tanzania Jenerali Venance Mabeyo
akikagua ngoma za asili katika sherehe za kumbukizi ya Mashujaa wa Vita vya
Majimaji vilivyopiganwa miaka 112 iliyopita amesema pamoja na kuenzi utamaduni
huo lakini kupitia Ngoma za asili na michezo vitaweza kuongeza Ajira kwa
Vijana.
No comments:
Post a Comment