Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Lodrick Mpogolo amesema
moja ya kuonyesha Mshikamano ni kufanya Ziara ya kutembelea Viongozi wa chini
kama Mabalozi kwa kuwafariji na kutatua
changamoto zinazowakabili.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa amesema anatamani kuona viongozi wote wachama wanashuka ngazi za chini kwenye mashina na mitaa kushughulika na shida za wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa amesema katika nguzo za chama cha Mapinduzi na kanuni zake chama kiliahidi kushughulika na shida za watu na watu hao wanapatikana katika mashina kwa mabalozi ambao ndio wanaofahamu changamoto za watu wao hivyo ili uwe kiongozi thabiti ni lazima kufanya kazi na mabalozi wenye wanachama.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Lodrick Mpogolo ameyasema hayo baada ya kumtembelea Mwanachama wa CCM Mzee Hashimu Awasi Bushiri wa Tawi la Mitopeni kata ya Mtina Tunduru kusini ili kufahamu anakabiliwa na changamoto zipi.
Katika Ziara hiyo ya kumtembelea Mzee Hashimu Bushiri Naibu Katibu Mkuu amewahamasisha wanachama wa CCM kujenga tabia ya kupendana na kusaidiana katika matatizo ili kudumisha umoja ndani ya chama cha Mapinduzi.
Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa ilizaa Matunda kwa Mzee Hashimu Bushiri ambaye baada ya kuona maisha
yake ameweza kupata ahadi ya kusaidiwa kukarabati Nyumba yake kwa kupiga bati nyumba
mzima pamoja na kumuekea umeme wa jua SOLA jambo ambalo Naibu Katibu Mkuu amesema kufanya hivyo ni
kuwapa moarari wazee waliokitumikia chama kwa muda mrefu.
Mwanachama wa CCM ambaye ni kamanda wa Zamani wa Umoja wa Vijana wilayani Tunduru Mzee Salehe Salehe amesema atahakikisha Mzee bushiri anabadili Maisha yake kwa kulala Nyumba yenye Bati na Kuondoa paa la Nyasi
Naye mwanachama Ferdinand Shitobera amehaidi mara baada ya kukamilika kupaua Bati katika nyumba ya Mzee Hashim Bushiri yeye atahakikisha mzee huyo anaishi katika nuru kwa kumuwekea SOLA ikiwa ni tuzo ya kukitumikia chama kwa muda mrefu sasa vijana wanarudisha fadhila kwa wazee waliokilea chama hicho.
Familia ya Mzee hashimu Bushiri wakitoa ushuhuda wa Maisha ya Mzee hashim wamesema amekua akihangaika muda mrefu kutokana na homa inayomsumbua ya kutetemeka mwili hana msaada wa kuweza kujikimu hivo kupata msaada kutengenezewa Nyumba kutamsaidia kubadili maisha yake.
Kati ya wanachama waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Naibu Katibu Mkuu Taifa ambaye alitoa shilingi laki moja (100,000) kumsaidia Mzee Bushiri wadau wengine wa CCM waliahidi kutoa misaada mbalimbali kwa mzee huyo.
Wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa katika kikao cha shina kikiongozwa na balozi wakati walipotembelewa na Naibu katibu Mkuu wa CCM Taifa kukagua utendaji kazi wa viongozi ngazi ya matawi katika Kata ya Mtina Jimbo la Tunduru kusini.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mtina wakisikiliza miongozo na kanuni za uendeshaji wa chama kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi Taifa amewataka Viongozi wa CCM kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya
Chama cha Mapinduzi kwa kuangalia miradi ya chama iliyoahidiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Lodrick Mpogolo ameyasema hayo wakati akipokea Pikipiki 15 zikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 33 zilizotolewa kwa Makatibu wa Kata wa chama cha Mapinduzi Jimbo la Tunduru kusini kwa ajili ya matumizi ya chama,
Katika Ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu amewapongeza wabunge wa Mkoa wa Ruvuma kwa kujali maslahi ya chama kwa kukisaidia chama kutoa vitendea kazi ameomba wabunge wengine wa CCM kuiga mfano wa Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini Mh. Daim Idi Mpakate ili kuimarisha chama.
Pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Tunduru kusini Mh. Daim Mpakate ili kurahisisha utendaji wa kazi za chama kwa kutembelea wanachama hadi kwenye Mashina
Katibu wa CCM Kata ya
Misechela akiongea kwa niaba ya Makatibu waliopewa Pikipiki hizo amesema
jiaografia ya wilaya ya Tunduru ni kubwa kupewa usafiri ni njia moja wapo ya
kurahisisha utendaji wa kazi.
Kati ya Kata 15 zilizopata Pikipiki ni pamoja na Mchuluka, Mchesi, Mchoteka, Misechela, Mbesa, Mtina, Ligoma, Nalasi Mashariki, nalasi Magharibi, Tuwe Macho , Mbati na Lukumbule zote zikiwa ni za Jimbo la Tunduru kusini Mkoani Ruvuma.
Umoja wa Machifu Tunduru Kusini wakiongozwa na Mzee Kalolo amewaomba Wazee kukishika chama cha Mapinduzi na kuacha uchochezi, amesema mara nyingine wapo wazee wamekuwa wakivuruga chama na kusababisha mitafaruku ndani ya chama jambo ambalo siyo busara kufanywa na wazee.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Daimu Idi Mpakate amesema ameamua kutoa Pikipiki hizo ili kuweza kuwasaidia wasimamizi wa chama waweze kutembelea Matawi na kushughulikia changamoto kwa uharaka
No comments:
Post a Comment