Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya nyasa Dr Osca
Mbyuzi ameyasema hayo wakati watumishi mbalimbali wa wilaya ya Nyasa walipo
shiriki michezo katika fukwe za Ziwa Nyasa ikiwa ni sehemu ya
kuboreesha Afya zao pamoja na kutii amri ya viongozi wa juu ya kutakiwa kufanya mazoezi
kila mwezi
Watumishi walio hudhuria katika mazoezi hayo ya michezo ya ufukweni wamesema licha ya kuboresha afya zao lakini michezo hiyo pia itaongeza uhusiano mzuri baina ya watumishi na wananchi
Nao Walimu wamsema michezo ya ufukweni itaongeza ari kwa wanafunzi kuja shuleni wakivutiwa na mpira wamiguu hasa baada ya kuona ushindani wao wanapo cheza mshindi hupewa mbuzi ambaye huchinjwa hapo hapo na wanafunzi kufanya kitoewo baada ya ratiba za michezo.
Waalimu kutoka Shule ya Uburcant wanasema wanatumia michezo kama motisha ya kuwafanya wanafunzi wanaopenda michezo wapende shule na kutokana na kuandaa mashindano ya mbuzi cup ambayo mshindi hupata kitoweo hivyo hakuna mwana funzi
anaye kosa michezoni
watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwa na Wananchi katika Mazoezi ya Viungo kando kando mwa Ziwa Nyasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dr Mbyuzi amesema siku zijazo Halmashauri itaandaa zawadi za aina mbalimbali kwa washindi watakaoshinda michezo ya ufukweni, Aidha amewaomba wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika michezo ya ufukweni kupitia fukwe nzuri za Mwambao wa Ziwa Nyasa.
Mazoezi ni sehamu ya kuimarisha Afya na Akili ya Binadamu lakini yasipozingatiwa ipasavyo inakuwa ni ugonjwa, Pichani watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakinyoosha viungo.
Michezo ya ufukweni iliyo
fanyika katika ziwa nyasa ili ambatana na michezo wa Mpira wa miguu wa ufukweni
,kufanya jogging,kukimbia mbio ndefu za ufukweni, kuogelea na zoezi la kukimbiza
mtumbwi
Miongoni mwa Michezo iliyofurahisha katika fukwe za ziwa Nyasa ni pamoja na mpira wa ufukweni ambao ulivutia watazamaji wengi.
Watumishi wa Halmashauri ya Nyasa wakisakata Boli la Ufukweni mubashara. |
No comments:
Post a Comment