Naibu Katibu Mkuu wa UWT
Taifa Eva Kiwele ameyasema hayo wakati alipotembelea Zahanati ya Libango na
kuwafariji wagonjwa , Naibu katibu Mkuu amesema Ujenzi wa zahanati na Kituo cha
Afya hii inaonyesha UWT inavyo jaliwa na serekari kwa kuwa huduma zitakazo tolewa maternity na theata ni miongoni mwa mikakati
ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.
Mhandisi wa Ujenzi
anayesimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Namtumbo ameeleza gharama zinazotarajia kutumika
mpaka ujenzi huo kukamilika, Katibu wa
UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro amesema kufika kwa Naibu Katibu Mkuu kutasaidia
kusukuma miradi iliyopo
Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya
Namtumbo Aloyce Mushi ameiomba Serikali
kuweka msukumo wa Upatikanaji wa wataalamu wa Afya katika idara ya upasuaji
pindi ujenzi wa Kituo cha Afya cha Rwinga Namtumbo
utakapokamilika. Jambo ambalo Naibu katibu mkuu amehaidi kulifikisha kwa Waziri wa Afya watumishi wapatikane haraka iwezekavyo ili huduma zianze kutolewa.
Wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa akina Mama UWT Namtumbo wakifurahi na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo nje ya Ofisi za chama cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo.Naibu katibu mkuu wa UWT Bi Eva kiwele amewaomba viongozi wa UWT kuhakikisha wanachama wao wanalipa Ada na kuwa wanachama hai kwa kuwa uhai wa Jumuia unatokana na wanachama kulipia kadi zao.
Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro akipokea maelekezo kutika kwa Naibu Katibu Mkuu ameahidi kutekeleza yale yote yaliyoelekezwa na kuhakikisha Jumuiya inakuwa Imara.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa alihitimisha ziara yake kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Piachani ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi Eva Kiwele akiwa na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Ruvuma na Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro
Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Ruvuma wakiwa nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Namtumbo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bi Lackness Amlima akiwa na ugeni ulioambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi Eva Kiwele walipotembelea Ofisini kwake.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa wa Ruvuma kutoka kulia ni Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro, anayefuata ni Mjumbe kamati ya Utekelezaji kutoka wilaya ya Tunduru Bi Yunus, Anayefuata ni Mjumbe kutoka wilaya ya Songea Bi Yusta Mwarabu na wa mwisho kushoto ni Pendo Ngonyani mwakilishi kutoka Namtumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo akisagana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mama Eva Kiwele
Wajumbe wa UWT wakiwa katika picha ya Pamoja, kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Namtumbo Matha Nikata na kulia wa mwisho ni Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro, katikati ni wajumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa waliokuwa wameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT katika ziara yake ya siku tatu wilayani namtumbo.
Huu ndio msimamo wa Utendaji kazi wilaya ya Namtumbo
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Namtumbo Matha Maiko Nikata amemweleza Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya UWT Taifa mikakati ya wanawake wa UWT wilaya ya Namtumbo kuwa ni pamoja na kujenga Jengo la kitega uchumi la Ukumbi ambao amesema ukumbi huo watautunuku jina la Naibu Katibu Mkuu EVA Kiwele.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Eva Kiwele amesema amesikitishwa baada ya kuona baadhi ya wanafunzi wakiwa wamevaa nguo zinazo ashiria ngono uzembe na wengine wakionyesha dalili za kuwa wajawazito na kuahidi hali hiyo ataifikisha kwa mheshiwa Rais amewaomba wazazi washirikiane na serekari kukemea vitendo hivyo ili wanafunzi waepukane na mimba za utotoni
Wanawake wa wa Kata ya Luegu
wamelalamikia ukosefu wa Maji safi ambayo imekua chanzo kikuu cha maradhi
ingawa mabomba yalishasambazwa lakini maji hayapatikani na kupelekea magonjwa
ya mlipuko kusambaa naKUSABABISHA watoto
wakike kubakwa wakati waKI tafuta maji .
Naibu Katibu Mkuu wa UWT
Taifa Eva Kiwele katika ziara yake wilayani Namtumbo alitembelea Zahanati ya Libango na
kuwafariji wagonjwa , na kupongeza jitihada za Serikali za kusogeza huduma za afya karibu na wananchi amesema jwepo wa zahanati na Ujenzi wa Kituo cha
Afya Namtumbo ni faraja kwa akina mama hii inaonyesha dhahiri UWT ina jaliwa na Seiekali kwa kuwa huduma zitakazotolewa za Maternity na theater ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika mikakati
ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.
Naibu katibu Mkuu wa UWT Taifa aliweza kutembelea eneo la mradi wa Uwanja wa UWT wilaya ya Namtumbo ambako wanatarajia kuwekeza katika Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano katika kuinua uchumi wa Jumuiya.Pamoja na kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo pia alisikiliza kero za wananchi katika kata ya Luegu na kufanikisha kutatua kero moja ya maji kwa kuendesha harambeed ya kuchangia fedha za kumalizia ujenzi wa mradi huo ili maji yapatikane.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Namtumbo Matha Nikata ameunga mkono suala la watoto wa kike kupata ujauzito ni
suala ambalo UWT wilaya ya Namtumbo itasimamia kutoa Elimu ili kumlinda motto
wa kike na mimba za utotoni.
Mhandisi wa Ujenzi
anayesimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Namtumbo ameeleza gharama zinazotarajia kutumika
mpaka ujenzi huo kukamilika, Katibu wa
UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro amesema kufika kwa Naibu Katibu Mkuu kutasaidia
kusukuma miradi iliyopo
Aidha Naibu katibu Mkuu Eva Kiwele akiweza kuwaingiza wanachama wapya wa UWT wanafunzi wa Sekondari katika Kata ya Luegu Wanafunzi waliojiunga na Jumuiya ya UWT Songea na kukabidhiwa kadi ya Jumuiya za uanachama wa UWT. Katika ziara hiyo pia Naibu katibu Mkuu hakuacha kuwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kujiepusha na kupenda vizawadi vidogo vidogo wakiwa shuleni kufanya hivyo ni kukaribisha kuvurugiwa mfumo wa maisha yao ya baadaye.
Wilaya za Namtumbo na Tunduru
zimekuwa ni wilaya ambazo zinaoongoza kwa watoto wa kike kuolewa mapema kabla
ya umri wao ambapo mikakati iliyowekwa na mkoa wa Ruvuma ni kuzingatia taratibu
za kuvaa magauni manne kwa kila gauni na wakati wake na kupiga marufuku kumuita motto wa kike Baby
au mrembo mtiririko sahihi wa magauni ni Sare ya Shule ya Msingi, Sekondari na
joho la chuo kikuu na kumalizia shela ya harusi.
Wilaya ya Namtumbo imekuwa na
changamoto ya watoto walio chini ya miaka 15 kuwa na watoto wenzao kuwepo kwa
zahanati na vituo vya Afya kutasaidia kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto. Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa amehitimisha
Ziara yake kwa kukagua miradi ya UWT ikiwemo kiwanja cha kujenga ukumbi, Ujenzi
wa Zahanati na Vituo vya Afya na kupokea kero za wananchi.Naibu katibu Mkuu akiwa ameshika kadi ya Mwanachama wa CUF aliyeamua kurudisha kadi na kujiunga na CCM. Ambapo akiwa kata ya Luegu aliweza kuingiza mwanachama mmoja na mwenyekiti wa Kitongoji kupitia chama cha CUF.
Katika kuwapokea wanachama hao Naibu katibu Mkuu alihamasisha ukarimu kwa wageni na kufanya harambee ya kuwapokea ambapo zilipatikana fedha kiasi ambazo walikabidhiwa wageni wakapate kitoeo ikiwa ni pongezi kwa kurudi nyumbani.
Naibu katibu Mkuu wa UWT Taifa amewapongeza waawake wa UWT wilaya ya Namtumbo amesema amefurahi sana kwa mapokezi yao mazuri na kuahidi kushirikiana nao katika maendeleo na kuwaasa kutumia zaidi mawasiliano katika kjazi taarifa ni muhimu ili kuondoa migongano na muingiliano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM wilaya ya Namtumbo Twaha akiongoza msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa.
Hizi ni nyumba ambazo alifikia Naibu Katibu Mkuu katika Hoteli ya ZIRO Namtumbo zenye mandhari nzuri wa kuvutia
Nyumba bora za kulala zinazopatikana Hoteli ya ZIRO wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma
Nyumba ya kulala wageni inayovutia ambayo ni Self Contained.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa amewataka wanawake kuwa
watekelezaji wa kusimamia Maadili badala ya kusimamia badala ya kugeuza Maadili
kama wimbo huku Vijana wakiendelea kupata madhara yanayotokana na mmomonyoko wa
maadili kama vile kupata Mimba
zisizotarajiwa.
Wanachama wa UWT wilaya ya Namtumbo wakimuonyesha Naibu katibu Mkuu Eneo litakalojengwa Ukumbi.
No comments:
Post a Comment