MRADI wa bustani ya Manispaa ya Songea umekamilika unatarajia
kuanza kufanyakazi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, ambapo Mkandarasi tayari
amekabidhi mradi huo kwa Manispaa.
Kaimu Mkuu wa Idara ya ujenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi
Nicolus Danda amesema mradi ulikamilika tangu Desemba 2017 ambapo Mkandarasi
alipewa matazamio ya miezi sita ya mradi huo
ambayo inaishia Aprili 2018.
Mradi wa Bustani ya Manispaa ya Songea umejengwa kwa ufadhili na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi milioni 399, hadi kukamilika mradi umetumia shilingi milioni 444.
Wawakilishi wa Benki
ya Dunia wameukagua mradi huo na kuridhishwa na kiwango cha ujenzi wake na kusema Bustani hiyo imebadilisha muonekano wa mji wa Songea.
Mradi wa Bustani ya Manispaa ni miongoni mwa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini
ya Mpango wa Kuzijengea uwezo serikali za mitaa (ULGSP).Ujenzi wa Bustani hiyo umehusisha eneo la mgahawa, choo cha kulipia, uzio, maeneo ya kupaki magari(parking bay), eneo la kupumzikia(resting huts) na maeneo ya kuchezea watoto, Pia kwa siku za baadaye bustani hiyo inatarajia kuwa na kituo cha kutolea Habari za Utalii na uwekezaji ndani ya Manispaa na Mkoa wa Ruvuma
No comments:
Post a Comment