Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea MRADI wa machinjio ya
kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni
tatu unaotarajia kukamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea katika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa inayojengwa kata ya Tanga manispaa ya Songea.
Mradi huo unaojengwa
katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea kwa sasa umefikia asilimia 80 ya
ujenzi wake, Mkandarasi wa ujenzi ujenzi huo Kampuni ya Giraffe ameahidi
kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo kabla ya tarehe ya mwisho wa mkataba ambapo mkataba wa ujenzi ulianza Julai
2017 na kukamilika Julai 2018.
Manispaa ya Songea imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma mbalimbali za wananchi ili kusogeza huduma karibu na wananchi Machinjio ya kisasa inayojengwa Kata ya Tanga itasaidia kuongeza Mapato ya Halmashauri ya Manispaa itakapoanza kutumika.Muonekano wa Majengo ya Mradi wa Machinjio hali ilivyo kwa sasa, Wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika biashara ndogo ndogo katika eneo hilo la Machinjio pindi mradi utakapokamilika.
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa unavyoendelea katika Kata ya Tanga Manispaa ya Songea.
No comments:
Post a Comment