WAKALA wa Majengo
Tanzania (TBA) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili
ya shule ya msingi Luhira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TBA kila bweni Lina uwezo wa kulaza wanafunzi 12 hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi wenye ulemavu 36.
Mkuu
wa shule hiyo Joyce Konga ameishukuru serikali kwa kuwajengea mabweni ya kisasa na
kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu, amesema shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 48 wenye
ulemavu na kwamba baadhi ya wanafunzi wenye umri mdogo watalazimika
kulala wawili wawili.
Shule ya msingi Luhira ndiyo Shule pekee yenye kitengo cha wasioona mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1929 na kitengo cha wasioona kilianzishwa mwaka 1982
Shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 1300 kati yao wenye ulemavu ni 48.Hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alitembelea shule hiyo na kukabidhi magodoro 24 yenye
thamani ya shilingi milioni 1.8 kwa ajili ya wanafunzi wasioona wanaosoma
katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment