Ni ukweli usiopingika kuwa furaha kubwa katika maisha ni kuwa na mtoto na kwa mzazi wa kike anaanza furaha ya mapenzi ya mtoto kbla ya kuzaliwa kwa mtoto lakini kwa baba furaha yake ya kwanza ni ile kuitwa baba hujikuta kuwa amepanda wadhifa fulani lakini baadhi ya wababa wanasahau kutimiza wajibu wao kwa watoto katika malezi jambo ambalo ni tofauti na mama.
Hakuna Mzazi ajuaye Kesho yake, ni wajibu wa kila mzazi kutengeneza maisha ya baadaye ya mwanae mara tu wanapokuwa katika matarajio ya kuzaliwa kwa mtoto kwani salio la maisha lipo mikononi mwa Mungu pekee. Pichani ni Bibie Sarah Gabriel akitabasamu kuashiria furaha ya kuingia katika malezi ya Mwanae kipenzi Hythamy ni wazi kuwa hata baba wa Mtoto ana furahi pia kumuona mtoto wake akiwa na bashasha Lakini Jee wanatambua wajibu wao kwa Mtoto katika kumtimizia mahitaji yake ya msingi na kutimiza ndoto zake?...!
Mtoto Hythamy akiwa na furaha haelewi lolote katika umri huu wa miezi mi nne akiwa ndo kwanza anayaanza maisha ya ulimwengu, jambo la muhimu kwa wazazi ni kufanya maandalizi mema ya kumtengenezea maisha mtoto wao katika malezi, elimu na msingi wa maadili mema. Siku hizi kumeibuka tabia ya wazazi kukwepa majukumu kwa watoto kwa kutotimiza wajibu wao na kupelekea wimbi la watoto wenye mmomonyoko wa maadili.
Turejee mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye ameanzisha kampeni ya kuwasaidia msaada wa kisheria wanawake waliotelekezewa watoto wao jambo ambalo halina hatia kwa watoto wetu, wazazi tunapaswa kujitathmini katika ili na kujiuliza sisi tumetoka wapi?
Aidha akina mama wanaotupa watoto wachanga ebu tumrudie Mungu jiulize mtoto kama huyo hapo juu ana kosa gani mpaka unamtupa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha au kutoelewana baina yenu wazazi tambua watoto hawausiki hawapaswi kabisa kupewa adhabu ya makosa ambayo hawakuwahi kushiriki hata punje wala kushuhudia malumbano ya mahusiano yenu.
No comments:
Post a Comment