KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 12, 2018

WAKALA WA MAJENGO TBA IMEKABIDHI MABWENI MATATU NA MADARASA MAWILI YA WASIOONA SONGEA


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili ya shule ya msingi Luhira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo na Manispaa ya Songea, Meneja wa TBA Mkoa wa Ruvuma Edwin Nunduma amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa mabweni matatu na ukarabati wa madarasa mawili kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 151
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TBA kila bweni Lina uwezo wa kulaza wanafunzi 12 hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi wenye ulemavu 36.

Mkuu wa shule hiyo Joyce Konga ameishukuru serikali kwa kuwajengea mabweni ya kisasa na kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu,  amesema shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 48 wenye ulemavu na kwamba baadhi ya wanafunzi wenye umri mdogo watalazimika kulala wawili wawili.

Shule ya msingi Luhira ndiyo Shule pekee yenye kitengo cha wasioona mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1929 na kitengo cha wasioona kilianzishwa mwaka 1982

Shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 1300 kati yao wenye ulemavu ni 48.Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alitembelea shule hiyo na kukabidhi magodoro 24 yenye thamani ya shilingi milioni 1.8 kwa ajili ya wanafunzi wasioona wanaosoma katika shule hiyo.

Tuesday, April 10, 2018

BUSTANI YA MANISPAA YA SONGEA KUANZA KUTUMIKA MWEZI MAY 2018


MRADI wa bustani ya Manispaa ya Songea umekamilika unatarajia kuanza kufanyakazi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, ambapo Mkandarasi tayari amekabidhi mradi huo kwa Manispaa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya ujenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Nicolus Danda amesema mradi ulikamilika tangu Desemba 2017 ambapo Mkandarasi alipewa matazamio ya miezi sita ya mradi huo  ambayo inaishia Aprili 2018.


Mradi wa Bustani ya Manispaa ya Songea umejengwa kwa ufadhili na Benki ya Dunia kwa  gharama ya shilingi milioni 399, hadi kukamilika mradi umetumia shilingi milioni 444.

Wawakilishi  wa Benki ya Dunia wameukagua mradi huo na kuridhishwa na kiwango cha ujenzi wake na kusema Bustani hiyo  imebadilisha muonekano wa mji wa Songea.
Mradi wa Bustani ya Manispaa ni miongoni mwa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa Kuzijengea uwezo serikali za mitaa (ULGSP).

Ujenzi wa Bustani hiyo umehusisha eneo la mgahawa, choo cha kulipia, uzio, maeneo ya kupaki magari(parking bay), eneo la kupumzikia(resting huts) na maeneo ya kuchezea watoto,  Pia kwa siku za baadaye bustani hiyo inatarajia kuwa na kituo cha kutolea Habari za Utalii na uwekezaji ndani ya Manispaa na Mkoa wa Ruvuma

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA SONGEA KUTEMBELEA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA KATA YA TANGA MANISPAA YA SONGEA


 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea MRADI wa machinjio ya kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu unaotarajia kukamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea katika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa inayojengwa kata ya Tanga manispaa ya Songea.
Mradi huo unaojengwa katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea kwa sasa umefikia asilimia 80 ya ujenzi wake, Mkandarasi wa ujenzi ujenzi huo Kampuni ya Giraffe ameahidi kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo kabla ya tarehe ya mwisho wa mkataba ambapo mkataba wa ujenzi ulianza Julai 2017 na kukamilika Julai 2018.
Manispaa ya Songea imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma mbalimbali za wananchi ili kusogeza huduma karibu na wananchi Machinjio ya kisasa inayojengwa Kata ya Tanga itasaidia kuongeza Mapato ya Halmashauri ya Manispaa itakapoanza kutumika.
Muonekano wa Majengo ya Mradi wa Machinjio hali ilivyo kwa sasa, Wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika biashara ndogo ndogo katika eneo hilo la Machinjio pindi mradi utakapokamilika.
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa unavyoendelea katika Kata ya Tanga Manispaa ya Songea.

Monday, April 2, 2018

IWaumini wa Dini ya Kristo Mkoani Ruvuma wametakiwa kudumisha amani pamoja na kuwajali watu wanao ishi katika mazingira Hatarishi wakati wakisherekea sikuu ya Pasakamin


 Mhashamu Asikofu Mkuu wa Kanisa la Redemed Assemblies of God Simoni   Silwimba amewataka waumini wa Dini ya kikristo kuwa jail watun wanao ishi katika mazingira hatarishi wakiwemo masikini ili wanapo sherekea sikukuu ya Pasaka nao masikini washereke
 Mhashamu Asikofu Mkuu wa kanisa ya Ruthiran  Dayosence ya Ruvuma Amoni Mwenda  amewaomba waumini wa Dini zote kudumisha Amani kwani ndiyo silaha pekee ya kuweza kjulinda Amani 

Mhashamu Asikofu Mkuu wa KKT Dayosence ya Ruvuma Amoni Mwenda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Kamando Mgema katika viwanja vya kanisa la KKT

WAaumini wa Kanisa la KKT Mkoani Ruvuma wakiwa katika ibada ya Pasaka
 Waumini wa kanisa katorik Mkoa wa Ruvuma wamewaomba waumuni wote kuendelea kufanya vitendo walivyo kuwa wakifanya wakati nwa kwaresima kuachana na ulevi,uzinzi, pamoja na kuachana na vitendo vya  na ufisadi
katibu wa Kanisa la UMSA ,Angilikani Maiko Mguyu amewataka waumini wakati wakfukarazingira magumu wakimo watoto,Masikini,na Maherekea sikukuu ya Pasaka wawa kumbuke na watu wanao ishi katika maus

Mchungaji wa Asembulies of God Gilida Silwimba amewataka wanawake kuongeza ushujaa kwakuwa wao ndio watu walio onyesha ushujaa kwa kwenda kudhuru kaburi la yesu na kuwa watu wa kwanza kumwona Yesu

Mzee Mwosha amewaomba waumini kufuata kanuni za za dini wakati wowote wamaisha yao
Mhashu Asikofu Mkuu wa Dayonsensi ya Ruvuma KKT Amoni Mwenda amewaomba waumini kushirikiana na Serekari katika kujenga Nchi ya Uchumi wa Viwanda ameya sema hayo katika ibada ya Misa ya PASAKA
Mhashamu Asikofu Mkuu wa Kanisa la Redemeede of Asemblies of Gog Simoni Suri ameya sema hayo wakati akihubiri siku ya Pasaka Mkoani Ruvumailwimba amewataka waumini kujua kuchomwa miba kwa Mkombozi Yesu Kristo ni swala la kuamusha ubongo wao ili waweze kupambanua mabaya na maz
binti Mdogo aliye anza kuimba nyimbo za injili akiwa Darasa la Nne lakini sasa amekuwa Mashuri kwa kuimba katika kanisa la Redeemede Asembulies of God