Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu akiwaasa wahitimu 822 wa Mafunzo ya awali ya Operation Maalum ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kikosi cha 842 KJ Mlale kutobweteka kwa kutarajia kupata ajira baada ya kupata Mafunzo ya JKT badala yake wayatumie Mafunzo hayo katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kazi za kujiajiri.
Mkuu wa Kikosi cha 842 KJ Mlale Meja Thomas Mpuku akitoa taarifa ya Jinsi Kikosi cha JKT kinavyojimudu na Mambo ya Uchumi hasa katika Sekta ya Kilimo. Msimu wa 2011/2012 JKT imeweza kulima Ekari 300 za Shamba la Kuzalisha Mbegu za Mahindi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua Gwaride Maalumu la Vijana wahitimu 822 wa Mafunzo ya awali ya Operation Maalum ya Miaka 50 ya Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu katikati akiingia katika Kambi ya Kikosi cha 842 KJ Mlale, Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Meja Thomas Mpuku, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Sabaya.
Bwana Shamba wa Kikosi cha Mlale Luteni Jackson Otaite akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu Mipaka ya shamba la uzalishaji wa Mbegu za Mahindi lenye Ukubwa wa Ekari 300 lijulikanalo jwa jina la Embakasi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akipokea Maelekezo kutoka kwa Bwana Shamba wa Kikosi cha JKT Mlale jinsi wanavyoweza kuzalisha Mbegu za Mahindi. Bwana Shamba huyo akionyesha tofauti kati ya Mahindi dume na jike.
No comments:
Post a Comment