KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo
Thursday, August 30, 2012
WAUGUZI NA MADAKITARI WALALA WODI ZA WAGONJWA
Baadhi ya watumishi wa idara ya afya wilayani mpwapwa walio ajiliwa
mwezi mei mwaka huu ambao ni manesi na matabibu wanalala kwenye wodi
za wagonjwa kwa muda wa miezi mitatu sasa kutokana na halmashauri
hiyo kuto kuwapatia nyumba na hela za kujikimu.
Kitendo hicho cha aibu na cha uzalilishaji kwa wataalamu hao
ambacho kimetokea kwa muda wa miezi mitatu sasa bila halmashauri hiyo
kuto kutoa majibu yeyote juu ya suala hilo.
Wakiongea na gazeti hili wilayani hapo baadhi ya watumishi hao
wamesema kuwa tangu waajiliwe mwezi mei mwaka huu halmashauri hiyo
iliwaonyesha wodi za wagonjwa kuwa walale kwa muda wakati
wanatafutiwa uataratibu wa malazi lakini mpaka sasa wamekuwa
wakiendelea kulala wodini hapo kama wagonjwa bila mkurugenzi huyo
kuchukua hatua za kuwalipa madai yao wala kuwalipa mishahara yao .
Aidha wamedai kuwa lalamiko hili wamelipeleka mpaka kwa mkurugenzi
mtendaji wa halimashauri hiyo lakini wamekuwa wakipigwa danadana
bila mafanikio, huku wakiambia waje kesho siku zikidi kusonga mbele
na kuendelea kupata shida
Watumishi hao ambao wengi ni manesi na maafisa tabibu ambao waliomba
majina yao yasiandikwe kwenye Blog ya songea Habari kwa usalama wa kazi zao walidai
kuwa tangu wafike katika halmashauri hiyo mwezi mei wanaishi maisha ya
kuomba omba kutokana na kuishiwa pesa za matumizi na inawalazimu
kulala wodini hapo kama wagonjwa huku wengine wakiwa wanategemea chakula kinachopikwa haosptali hapo kwa ajili ya wagaonjwa walio
lazwa hospitali hapo,
Akiongea mmoja wa watumishi hao huku akitokwa na machozi alisema kuwa
tangu waajiliwe wakuu wa idara hiyo na ofisi ya mkurugenzi
wamekuwa wakisingizia mfumo wa sasa wa utoaji malipo kwa watumishi
ujulikanao kama EPICOR unawakwamisha kuweza kuwalipa watumishi hao
kitu ambacho baadhi ya watumishi hao walipingana nacho
P ia wakiongea zaidi walidakuwa baadhi ya watumishi wenzao wa wilaya
zingine walio ajiliwa nao walisha lipwa pesa zao za kujikimu na
tayari walisha anza kupokea mishahara ya ‘ iweje kwa mpwapwa tu
inamaana mpwapwa ndo inatumia epicor ya kwao peke yao”walihoji
watumishi hao .
Akiuliozwa juu malalamiko hayo mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya
wilaya ya mpwapwa FANUEL SENGE alikili kuwepo kwa matatizo hayo na
alisemakuwa mfumo huo wa LONSON ndio imesababisha kushindwa
kuwalipa watumishi hao .
Alipoulizwa kuhusu watumishi hao kulazwa wodi ni kama wagojwa
mkurugenzi h uyo alikanusha alisema kuwa hili halijui isipokuwa
ataongea na mkuu wa idara ambae ni mganga mkuu wa wilaya bwana
MOHAMED PATHAN.
Utafiti uliofanywa na Blog ya Songea Habari hapo wilayani hapo umegundua kuwa
halimashauri hiyo imekosa wataalamu wazuri wa IT kitu kinacho wapelekea baadhi ya watumishi kushidwa kulipa madeni yao na
mishahara kuchelewa kutoka kwa watumishi wote kwa miezi miwili mfululizo sasa kutokana na mfumo huu wa EPICOR.
JUMA NYUMAYO APATWA NA MSIBA MKUBWA SONGEA
Nasibu Nyumayo akiwa anaingia kaburini ili kumzika mke wake ambaye alifarikikatika hospitali ya Mkoa Ruvuma
Ally Jaibu akitoa maelekezo baada ya Mazishi na kuweza kulishukuru jeshi la wananchi wa Tanzania kwa jinsi walivyo weza kushiriki kwa Hali na Mali
Watu wakiendela kuombeza kifo cha mrs Nyumayo huku wakiendelea kumimi nika kushiriki mazishi
Wazikaji wakiwa ndani ya Kaburi kuhakikisha Mwandani umekaa vizuri wakiongozwa na Nasibu Nyumayo mume wa Marehemu
Wanawake walio shiriki eneo la msiba wakikumbuka mwenzao walipo kuwa naye Hai
Waislamu waliswali sala ya Jeneza mbele ya nyumba Mama mzazi wa ukuoo wa akina Nyumayo
Sunday, August 26, 2012
MTOTO AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI - SONGEA
Kwa mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume Joseph Mapunda pichani hapo juu kutembea na mama yake mzazi. Wana Ruvuma wanauliza tume jikwaa wapi watanzani hadi kupoteza mila desturi na maadili ya mtanzania pia kukiuka sheria za dini
Saturday, August 25, 2012
NDOA RAHISI AMBAYO KILA MMOJA ANAWEZA KUIMUDU
Thursday, August 23, 2012
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WAOMBA MSAADA WA ULINZI KATIKA MABWENI YA WASICHANA
Adam Nindi Songea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wameiomba Serikali kuwaongezea ulinzi kutokana na kuingiliwa na Wanaume nyakati za usiku.
Mkuu wa Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Songea Janemary Mwinyikombo amesema tabia ya kuvamia mara mara na wanaume imeongeza hofu ya wanafunzi na kusababisha wanafunzi kushindwa kujisomea nyakati za usiku.
Kiranja Mkuu wa Shule ya sekondari ya wasichana songea Janemary Mwinyikombo akiwa na Katibu Bernadetha Mathew Pamoja na Wanafunzi waliofanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kuchaniwa nguo kwa wembe na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Ankol .ambaye mara kwa mara huingia kwa njia ya kimazingira wamesema hali hiyo inawakosesha raha shuleni hapo
Wamesema pamoja na wanafunzi kufunga milango na kupigilia misumari kwenye madirisha lakini cha kushangaza wanaume hao huingia na kuchana nguo za wasichana maeneo ya kifuani, wamesema hali hiyo hutokea kuanzia saa 7.00 usiku na pale wanapo ingia wanafunzi hukumbwa na hali ya kushindwa kusema.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekonndari ya wasichana Songea Welinald Riki Liwiki amekiri kuwepo kwa Vitendo hivyo na amesema ameongeza ulinzi, yeye mwenyewe pia anashiriki ulinzi, ameomba Jamii kushirikiana na shule katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo kwa wanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana songea amesema katika hali ya ulinzi wa usiku kwa kuwa naye hushiriki siku moja alinusurika kuuwawa na mlinzi baada ya mlinzi kufikili yeye ndiye mwanaume anaye waingilia wanafunzi kimazingira
Shule ya sekondary ya wasichana songea kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na vitendo vya wanaume kuwaingilia wanafunzi kimazingira ingawa hali hiyo bado ni tata wanafunzi a secondary ya wasicha wameomba jamii na wazee wa mila kukaa na kuweza kulitatua tatizo hilo vinginevyo itasababisha wanafunzi kuathirika zaidi kisaikolojia jambo litakalo sababisha elimu kuteremuka
Tuesday, August 21, 2012
ALIYE TELEKEZA MTOTO SONGEA AKAMATWA NA JESHI LA POLICE
Jeshi la police lilipo mhoji Zawadi Komba 18 alidai siku hiyo alikuwa akifukuzwa na kichaa ndipo alipo mtupa mtot lakini baada ya kubana na mkono wa sheria ndipo alipo eleza ukweli kuwa alitumbukia katika dimbi la mapenzi
Sunday, August 19, 2012
WAISLAMU WAASWA KUDUMISHA AMANI NA KUFUATA MAAMURISHO YA MWENYEZI MUNGU KWA KUTENDA MAMBO MEMA
Mkuu wa Mkoa wa
Sheikh Mkuu Nchini
Katika Misikiti mbalimbali Mkoani Ruvuma waumini wote kwa ujumla wameiombea Nchi yetu kuwa na Viongozi bora wenye kujali Watanzania na sio kujali Maslai
Mkuu wa Mkoa wa
Sheikh wa dhehebu la Ahamadiya Mkoa wa Ruvuma Yusufu Kambaulaya amesema wanaruvuma tunatakiwa kumuombea Rais wetu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete aendeleze amani kwa Nchi tunazopakana nazo, pia waumini wameomba waislamu washiriki Sensa ya watu na makazi.
Thursday, August 16, 2012
RAIS WA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII AWAMU YA TATU


Wednesday, August 15, 2012
MTOTO ATUPWA JALALANI ENEO LA MITUMBANI SONGEA
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Anna Tembo amewataka wanawake wa Mkoa wa Ruvuma kuwa na huruma kwa watoto wanaowazaa sifa ya kwanza ya mama ni kuwa na upendo na huruma kwa watoto.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Inspekta Anna Tembo ameyasema hayo baada ya Mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 5 kutelekezwa kwenye Ghuba ya takataka eneo la Majengo Manispaa ya Songea.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo amesema kitendo cha mtoto mdogo kumtelekeza kwenye jalala ni sawa na Mtoto huyo kuwatupia Mbwa wamle hiyo ni kukosa sifa halisi ya Mama.
Anna Tembo amesema Mtoto huyo wa kiume ambaye aliokotwa kwenye Jalala katika manspaa ya songea Majengo anahifadhiwa na Mama mmoja ambaye amejitolea kumtunza. Mtoto huyo hana nguo, anahitaji chakula ambacho ni Maziwa mwenyekiti amewaomba wasamalia wema wajitokeze kumsaidia kupitia Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma.
. Mama ambaye amejitolea kumtunza Mtoto huyo wa kiume Futuma Ndimbangi amesema usiku wa saa moja jioni aliitwa na shemeji yake na kumtaka aende na taa nje walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto akilia kutokana na baridi pia alionyesha kuishiwa nguvu alipo pelekwa hospitali alionyesha kuwa hajala kwa muda mrefu.
Mkoa wa Ruvuma ambao ulisifika kwa huruma kwa wageni na kusifiwa kwa kutunza watoto sasa umeingia kwenye adha ya ukandamizaji kwa kutesa watoto, katika mwezi mmoja zaidi ya watoto 3 wameokotwa na watoto wawili kuuwawa na mama zao ambao kesi zao zipo Mahakamani.