Na noel Stephen mpwapwa Dodoma
Baadhi ya watumishi wa idara ya afya wilayani mpwapwa walio ajiliwa
mwezi mei mwaka huu ambao ni manesi na matabibu wanalala kwenye wodi
za wagonjwa kwa muda wa miezi mitatu sasa kutokana na halmashauri
hiyo kuto kuwapatia nyumba na hela za kujikimu.
Kitendo hicho cha aibu na cha uzalilishaji kwa wataalamu hao
ambacho kimetokea kwa muda wa miezi mitatu sasa bila halmashauri hiyo
kuto kutoa majibu yeyote juu ya suala hilo.
Wakiongea na gazeti hili wilayani hapo baadhi ya watumishi hao
wamesema kuwa tangu waajiliwe mwezi mei mwaka huu halmashauri hiyo
iliwaonyesha wodi za wagonjwa kuwa walale kwa muda wakati
wanatafutiwa uataratibu wa malazi lakini mpaka sasa wamekuwa
wakiendelea kulala wodini hapo kama wagonjwa bila mkurugenzi huyo
kuchukua hatua za kuwalipa madai yao wala kuwalipa mishahara yao .
Aidha wamedai kuwa lalamiko hili wamelipeleka mpaka kwa mkurugenzi
mtendaji wa halimashauri hiyo lakini wamekuwa wakipigwa danadana
bila mafanikio, huku wakiambia waje kesho siku zikidi kusonga mbele
na kuendelea kupata shida
Watumishi hao ambao wengi ni manesi na maafisa tabibu ambao waliomba
majina yao yasiandikwe kwenye Blog ya songea Habari kwa usalama wa kazi zao walidai
kuwa tangu wafike katika halmashauri hiyo mwezi mei wanaishi maisha ya
kuomba omba kutokana na kuishiwa pesa za matumizi na inawalazimu
kulala wodini hapo kama wagonjwa huku wengine wakiwa wanategemea chakula kinachopikwa haosptali hapo kwa ajili ya wagaonjwa walio
lazwa hospitali hapo,
Akiongea mmoja wa watumishi hao huku akitokwa na machozi alisema kuwa
tangu waajiliwe wakuu wa idara hiyo na ofisi ya mkurugenzi
wamekuwa wakisingizia mfumo wa sasa wa utoaji malipo kwa watumishi
ujulikanao kama EPICOR unawakwamisha kuweza kuwalipa watumishi hao
kitu ambacho baadhi ya watumishi hao walipingana nacho
P ia wakiongea zaidi walidakuwa baadhi ya watumishi wenzao wa wilaya
zingine walio ajiliwa nao walisha lipwa pesa zao za kujikimu na
tayari walisha anza kupokea mishahara ya ‘ iweje kwa mpwapwa tu
inamaana mpwapwa ndo inatumia epicor ya kwao peke yao”walihoji
watumishi hao .
Akiuliozwa juu malalamiko hayo mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya
wilaya ya mpwapwa FANUEL SENGE alikili kuwepo kwa matatizo hayo na
alisemakuwa mfumo huo wa LONSON ndio imesababisha kushindwa
kuwalipa watumishi hao .
Alipoulizwa kuhusu watumishi hao kulazwa wodi ni kama wagojwa
mkurugenzi h uyo alikanusha alisema kuwa hili halijui isipokuwa
ataongea na mkuu wa idara ambae ni mganga mkuu wa wilaya bwana
MOHAMED PATHAN.
Utafiti uliofanywa na Blog ya Songea Habari hapo wilayani hapo umegundua kuwa
halimashauri hiyo imekosa wataalamu wazuri wa IT kitu kinacho wapelekea baadhi ya watumishi kushidwa kulipa madeni yao na
mishahara kuchelewa kutoka kwa watumishi wote kwa miezi miwili mfululizo sasa kutokana na mfumo huu wa EPICOR.
No comments:
Post a Comment