Adam Nindi, Songea
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Anna Tembo amewataka wanawake wa Mkoa wa Ruvuma kuwa na huruma kwa watoto wanaowazaa sifa ya kwanza ya mama ni kuwa na upendo na huruma kwa watoto.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Inspekta Anna Tembo ameyasema hayo baada ya Mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 5 kutelekezwa kwenye Ghuba ya takataka eneo la Majengo Manispaa ya Songea.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo amesema kitendo cha mtoto mdogo kumtelekeza kwenye jalala ni sawa na Mtoto huyo kuwatupia Mbwa wamle hiyo ni kukosa sifa halisi ya Mama.
Anna Tembo amesema Mtoto huyo wa kiume ambaye aliokotwa kwenye Jalala katika manspaa ya songea Majengo anahifadhiwa na Mama mmoja ambaye amejitolea kumtunza. Mtoto huyo hana nguo, anahitaji chakula ambacho ni Maziwa mwenyekiti amewaomba wasamalia wema wajitokeze kumsaidia kupitia Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma.
. Mama ambaye amejitolea kumtunza Mtoto huyo wa kiume Futuma Ndimbangi amesema usiku wa saa moja jioni aliitwa na shemeji yake na kumtaka aende na taa nje walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto akilia kutokana na baridi pia alionyesha kuishiwa nguvu alipo pelekwa hospitali alionyesha kuwa hajala kwa muda mrefu.
Mkoa wa Ruvuma ambao ulisifika kwa huruma kwa wageni na kusifiwa kwa kutunza watoto sasa umeingia kwenye adha ya ukandamizaji kwa kutesa watoto, katika mwezi mmoja zaidi ya watoto 3 wameokotwa na watoto wawili kuuwawa na mama zao ambao kesi zao zipo Mahakamani.
No comments:
Post a Comment