Waziri wa
Maliasili na Utalii Nchini Tanzania Balozi Hamis Kagasheki ameweza kuongoza
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji
walionyonga tar 27/02/1906 na Wajerumani ambapo Mashujaa 61 walizikwa katika
Kaburi moja.
- Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki.
Hapo Mh.
Balozi Hamis Kagasheki akiongoza Maandamano yaliyoanzia Sehemu waliyonyongwa
hadi katika Uwanja wa Mashujaa
- Katika Maombolezo yaliyofanywa Viwanja vya Mashujaa Mahenge Mgeni Rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki aliweza kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, hapo anaonekana akiweka Ngao.
- Waziri wa Maliasili Balozi Hamis Kagasheki akienda kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mahujaa Mahenge.
Mkuu wa mkoa akirudi jukwaani baada ya kuweka silaha ya jadi aina ya kinjenje
Bregedia akiwa katika mnara wa Mashujaa Mahenge akiweka Upinde na Mshale
- Chifu wa Wangoni Mbano akiwakilisha Wangoni kwa kuweka Kinjenje na Rungu (Kibonga) katika Mnara wa Mashujaa
- Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
Hiyo yote ninjia ya kuwakumbuka Mashujaa walio Tangulia
Ukiwa umepitia mafunzo ya kijeshi utajua uchungu wanao upata waombolezaji hawa
Nimoja ya kuomboleza kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa walioo tangulia Mbele zahaki
Jeshi unatakiwa kungangamala ,hebu ona jinsi mashujaa wanavyo omboleza katika kuwa kumbuka Mashujaa waliotangulia
Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wakiwa katika viwanja vya mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea
Jeshi la
Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya
kumaliza taratibu zote za
Maombolezo kwa kuwakumbuka Mashujaa 61
walionyongwa na kuzikwa katika
kaburi moja
Mwalimu Kaisi Ally kutoka dhehebu la Ahamadiya Mkoa wa Ruvuma akiwaombea mashujaa walio Tangulia wakati wa maombolezo katika uwanja wa mashujaa manispaa ya songea
Mkuu wa
Wilaya ya Rudewa Juma Madaha akiwa mmoja wa waombolezaji wa
Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya
Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya
Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya
Majimaji.
No comments:
Post a Comment