Adam Nindi, Songea.
Jeshi la Polisi
Mkoani Ruvuma limewataka Madereva wote wanaoendesha Mabasi ya Abiria kuwa na
Tahadhari wakati huu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya ili kuepusha ajali
ambazo zinaweza kuepukika.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki akieleza hali halisi ya ajali katika mkoa wa Ruvuma kwa mwakla 2012 na 2013 ameanisha kama
ifuatavyo
Kwa kipindi cha Mwaka
2013 hadi mwezi November jumla ya Ajali zilizotokea ni 454
zilizosababisha vifo 111
. Ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo jumula ya
ajali zilikuwa 537 zilizo sababisha vifo vya watu 93
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema
Ajali nyingi hutokea kutokana na Abiria kushabikia Mwendo mkali kwa Madereva
pia Madereva kutokuwa waangalifu katika sehemu tete zinazosababisha ajali mara
kwa mara.
No comments:
Post a Comment