KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo
UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Monday, December 9, 2013
MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA NA WAASISI WAJUTIA KUKOSA PENSHENI YA UZEENI
Mwasisi wa Chama cha TANU na CCM Mzee Mustafa Mohamed Songambele akieleza changamoto zilizopatikana mpaka kutimiza miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, Amesema alizaliwa tarehe 25/5/1925 katika kata ya Bombambili Mkoani Ruvuma, alianza shule ya Msingi 1932 na kumaliza mwaka 1936 akiwa darasa la Nne, baada ya kumaliza masomo ya shule ya msingi aliamua kwenda mkoa jirani wa Iringa safari ili kuwa ya kutembea kwa mguu kutokana na kukosa nauli. Alipofika Mkoa wa Iringa alijifunza udereva na hatimaye alihamia Dar -es -salaam ambako alikuwa mkuu wa Madereva mwaka 1969
Aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Ilala hatimaye kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar -es salaam hadi mwaka 1994 akiwa mkuu wa mkoa wa Tabora, baada ya hapo aliajiriwa na shirika la Tanesco aliko sitahafu
Mzee Mustafa Mohamed Songambele akiwa na Waandishi wa Habari amesema kuwa katika miaka yote aliyofanya kazi chini ya chama kimoja Mpaka leo hajafikiriwa kuhusu Pensheni na hategemei kama atapata Pensheni alisema kwa kushangaa.
Mzee Songambele amesema ikiwa yeye aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hatimaye kuwa Mkuu wa Mkoa hapati Pensheni, jee mkulima wakawaida atapata pensheni ya kilimo ? ni maajabu alisema, Amesema kazi ya Serikali hivi sasa ni kutoa Nishani za Chama ambazo hazina fedha, wakati mwingine ukifa hapo Serikali hujitokeza na kusema huyu alikuwa mtu mashuhuri wakati mwingine kujenga minara mikubwa ambayo haina maana kwa marehemu, Mfano mzuri ni mama Forodhani wa Songea Mwasisi wa TANU na CCM ambaye alipigania uhuru baada ya kufa ndipo nyumba yake ina karabatiwa ina maana gani kwa marehemu
Mwasisi wa TANU na CCM Mzee Mustafa Mohamed Songambele akionyesha jinsi alivyo fanya kazi, mbele yako ni Leseni ya Udereva aliyo ipata 24/9/1945 . Pamoja na hayo yote hakufikiriwa pensheni hadi leo anasema ni vizuri serikali kupunguza kuwasifu wafanyakazi bali wawaongezee uwezeshaji ili waweze kuishi maisha salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment