Kiongozi Mbio za Mwenge kitaifa Racher Stephen Kassanda amesema wahamiaji walio wengi kutoka Eretria, Somalia hupitia Mipaka ya Mkoa wa Ruvuma.
Pichani anayehutubia ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2014, anayefuatia katikati ni Afisa uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza na wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti.
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru katika Jengo la Makaazi la Afisa Uhamiaji lililozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Racher Stephen Kassanda. Pichani aliye katikati ya viongozi wa Mbio za Mwenge ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza.
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Mbio za Mwenge mara baada ya kuzindua Jengo lao.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akisoma Risala kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesema lengo la kujenga nyumba za makazi na kuzikarabati ni kuondoa changamoto zinazokabili wafanyakazi wa Uhamiaji wanapokuwa nje pia kuleta ufanis katika kazi.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Ruvuma
umeweza kuzindua Miradi mbalikmbali katika wilaya za Nyasa, Mbinga na wilaya ya Songea
ambapo miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na kuzindua Jengo la Makaazi la Uhamiaji lililogharimu shilingi
434,100,170. Mwenge unaendelea na Mbio zake katika wilaya ya Namtumbo na
Tunduru.
Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Shaban Shaban akiwa tayari kupokea Mwenge wa Uhuru katika eneo la Jengo la Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma. |
Katika Utunzaji wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Racher Kassanda aliweza kupanda Mti wa mkungu akiashiria kushiriki katika utunzaji wa mazingira.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza Akipokea Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya Uzalendo ya Nchi ya Tanzania.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kushoto ni Bw Shaban Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma
Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma lililozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Lililogharimu kiasi cha Shilingi 434,100,170. Lililopo Mahenge Manispaa ya Songea.
Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akisoma Taarifa ya Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Makazi ya Afisa Uhamiaji kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma akiwa na Ma WP wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa ruvuma katika eneo lililofanyika uzinduzi wa Nyumba ya Makazi iliyozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2014. |
Mwasibu wa Idara ya Uhamiaji aliyeshika Mwenge katika eneo la Jengo la Makaazi la Uhamiaji.
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika eneo la Jengo la Uhamiaji wakisubiri kwa hamu kushuhudia Uzinduzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji lililozinduliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Racher Kassanda July 2014
No comments:
Post a Comment