Ndugu msomaji unafahamu faida za uzazi na matatizo yanayotokana na Uzazi hasa ikiwa ukuzingatia maagizo ya wataalamu wa Afya. Huyo unayemuona ni Muuguzi Mkuu wa Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Mkoa akitoa Elimu ya Malezi ya watoto na kuelimisha dalili za hatari kwa watoto wachanga na wazazi waliotoka kujifungua ambazo zinapojitokeza Mzazi anapaswa awahi katika Kituo cha Afya kilicho karibu naye. Elimu hiyo alikuwa akiitoa kwa Wazazi 30 waliojifungua siku hiyo.
Wazazi pamoja na kubeba jukumu la kutakiwa kuongeza familia tunatakiwa kutambua athari za uzazi usio wa Mpango wataalamu siku zote wanashauri kuzaa kwa mpango idadi ambayo utaweza kumudu kuihudumia mahitaji ya msingi. Mama unayemuona hapo amejifungua watoto mapacha katika Hospitali ya Mkoa wa ruvuma na huo ni uzazi wake wa tano. Jee ingekuwa wewe huyo ni mkeo ungetoa ujshauri gani ili kumsaidia kiafya na Malzi bora ya Familia?
Kikundi cha Akina Mama wa Kipare na walioolewa na wapare waishio Manikspaa ya Songea baada ya kuguswa na uchungu wa Uzazi na kwa kutambua adha wanazozipata akina mama katika uzazi waliamua kuchangishana pesa toka mifukoni na Kununu zawadi ya sabuni zenye thamani ya sh. laki mbili na kutembelea wazazi waliojifungua na wanaotarajia kujifungua na kuwafariji kwa kuwapa zawadi ya Sabuni ili iwasaidie kidogo kwa kufanyia usafi maana Mzazi anapokuwa katika hali ya kulea au kutarajia kuanza ulezi anahitaji usafi wa hali ya juu kwa usalama wa afya yhake na ya mtoto. Hapo akina mama wakiwa getini wakimsubiri muuguzi awaongoze kuelekea wodini kutimiza lengo lao.
Siku hizi kuna watu wengi ambao wana uwezo na hujitolea sana katika starehe mfano katika Harusi, Send Of, Kitchen part na hata Majamanda sehemu ambazo watu hutoa kwa kushindana lakini wanasahau kama kuna watu wenye mahitaji ambao hawana uwezo na wanahitaji faraja. Hebu tuige mfano wa akina mama hao ambao hawana shughuli lakini wamejikuta wakiwa na huruma na kutembelea makundi maalumu kama Kituo cha watoto Yatima, na Hospitali kuwafariji wazazi wenzao na Mungu atawabariki. Jee wewe unayekesha baa na kutumia pesa nyingi au unatoa katika mambo mengine ya anasa kwa nini usitumie kiasi kingine kutoa kwa watu wasio na uwezo kama walikvyofanya wamama wa kipare waishio Songea?
Aina Mama wakipare wakiwa na Muuguzi wa Wodi za Uzazi katika Hospitali ya Mkoa akiwaongoza kwenda kutoa kidogo walichokusudia kukitoa kwa wazazi wenzao. Jee ndugu msomaji jiulize Mungu amekupa Kipato Kiasi gani na umetumia katika kusaidia Watu gani. Na kwanini alikupa wewe na akawanyima wengine?
Akina mama wa kipare na walioolewa na Wapare wanaoishi Manikspaa ya Songea wakiongozwa na Mama wa Nikdhamu wakifurahia kwenda kuwafariji wazazik wenzao kwa Sabunik ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuwapongeza kwa kukubali kutimiza Jukumu walilojaliwa na Mwenyezi Mungu la kuongeza familia na kulea.
Bi Fatujma Swai mmoja wa wanakikundi cha Akina mama wa kipare ambacho huwezeshana katika majanga na kufariji makundi mbalimbali yanayohitaji faraja. Hapo ni Wodi ya Wazazi wanaosubiri kujifungua wakiwapa zawadi ya sabuni ikwasaidie kidogo kwa kufulia nguo zao.
Mzazi aliyejifungua akipokea sabuni na kushukuru kwa faraja toka kwa akina mama hao wa Kikundi cha kuwezeshana cha wapare na walioolewa na wapare waikshio Manikspaa ya Songea. Mama huyo amesema ameshukuru sana kwa moyo huo ameomba na wengine wenye nafasi waige mfano huo wa kuwakumbuka wagonjwa. Amesema kwa upande wake yeye ni mwenyeji wa Mbinga lakini toka alipofika Hospitalini hapo na kulazwa ana zaikdi ya wiki moja lakini hajawahi kutembelewa na ndugu yeyote wala rafiki yeyote aliyethubutu kumletea choichote hivyo amefarijika sana leo kupata sabunik ya kuweza kumsaidia kufanyia usafi atapumzika kuomba kwa wenzake amb ao walikuwa wakimsaidia siku zote.
Mama wa Kipare akifurahi na Mtoto aliyezaliwa siku baada ya kutoa zawadi ya sabuni amesema amejisikia faraja kutembelea siku hiyo katika wodi ya wazazi kwani na yeye siku hiyo ndiyo aliyozaliwa na kuingia duniani hivyo ametoa zawadi hizo huku naye akifurahia kuzaliwa kwake pamoja na watoto wote waliozaliwa tarehe ambayo naye alizaliwa.
Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo inakabiliwa na Msongamano wa Wazazi katika wodi za Uzazi na hata wazazi wengine kulazimika kulala kitanda kimoja wazazi wawili, wamepata bahati ya kutembelewa na Akina Mama wenye moyo wa Huruma na na wenzao. Pichani ni Mwenyekiti wa Kikundi cha LUKUNDONYIKANAVA CHEE kikundi cha akina Mama wa Kipare Mama Mbaruku akitoa maelekezo kwa wanakikundi kuhusu wodi watakazozitembelea kutoa zawadi.
Kikundi cha akina Mama wa Kipare wakiwa Nje ya wodi za Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma muda mfupi baada ya kutoa zawadi katika wodi za wazazi wanaosubiri kujifungua, wodi ya wazazi waliojifungua kawaida na wa oparesheni na wodi ya wazazi waliojifungua watoto wa maangalizi maalum (Njiti) ambako walikfanikisha kutoa sabuni kwa kila mzazi mwenye mtotot mmoja nche mmoja na walio na mapacha miche miwili 2
Akina mama wa Kikpare hapo wakitoka wodini kutoa zawadi za Sabuni kwa wazazi wenzao.
Ndugu msomaji nadhani unafuatilia vyombo vya habari na taarifa mbalimbali juu ya vitendo vya unyanyasaji wa akina Mama na Watoto ama ukatili wa kijinsia vitgendo ambavyo vinapingwa na kupigiwa kelele siku zote. Vitendo hivi pia vimeikumba na jamii ya Mkoa wa Ruvuma kumekuwa na matukio mbalimbali ya kutupa vichanga na ukatili wa aina nyingine kama wazazi kunyonga watoto wao, kupiga kupita kiasik n.k. kutokana na ugumu wa maisha, na unafahamu ugumu wa malezi ya familia inapotokea mzazik mwenza anakutelekeza, kwa nini usione fahari kusaidia japo kikdogo ulichonacho kwa kundi hili la wazazi ili kuwapa moyo na faraja ya kuwafanya wasiwe na mawazo ya kutupa au kuuwa viumbe visikvyo na hatia? Sikuzote tukumbuke ukitoa na Mungu atakubariki zaikdi.
Mzazi aliyejifungu Muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Mkoa akifurahia zawadi na huduma nzuri ya wauguzi wa Hospitali ya Mkoa hasa kwa kuwapa elimu ya Malezik na jinsik ya kutambua dalili hatarishi za mtoto na mzazi anaporudi nyumbani ambazo atatakiwa awahi kukimbia hospitali kupata matibabu.
Wanakikundi cha LUKUNDONYIKA NAVACHEE Bi Fatuma Swai na B i Swaumu wakiwa na furaha kubwa baada ya kutimiza dhamira yao ya kuwafariji wazazi waliojifungua walioko katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
Jamii inatakiwa itambue kuwa kila jambo lina heri kwa Mwenyezi Mungu hasa unapotoa kwa moyo kidogo ulichonacho lazima na Mungu atakupa ili uweze kusaidia waliokosa kukipata. Jambo walilolifanya Akina Mama hao ni la thawabu kubwa hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Nani Kama Mama? Kwa kweli Mama anahitaji faraja na kupongezwa kwa kazi ngumu aliyopewa na Mwenyezi Mungu tgangu uzazi hadi malezi. Ndugu Msomaji jiulize Mungu amekupa uwezo kiasi gani na nanik aliyekufanya uzaliwe, ukue na kufikia umri wa kujitambua, Jee unadhani ni halali kumdharau Mama tafadhali tuige mfano wa kikundi hiki cha akina Mama ambao sik shirika wala Serikali lakini wameweza kutembelea Watoto Yatima wa Kituo cha Yatima Chipole na baadaye kutembelea Wodi ya Wazazik wa Hospitali ya Mkoa kutoa faraja kwa wenzao Kikundi amb acho hakina Mrfadi wowote. Jee wewe na Mimi tunasubiri nini na tumejaliwa kiasi Gani. kama si wewe muelimishe mwenye nafasi atoe kwa wasiojiweza.
Hapo akina Mama wakiwa katika Geti la Kuingia Wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakisubikri kuingia katika Wodi ya Wazazi kwenda kutoa Sabuni kwa Wazazi wenzao.
Akina Mama wakiwa wamebeba Sabuni wakisubiri kuongozwa Wodi ya Wazazi kutoa zawadi kwa akina Mama waliolazwa Matenity.
Kulia ni Mc wa kikundi cha Akina Mama wa kipare na walioolewa na Wapare akiongoza Msafara wa Wanakikundi kuelekea Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Mkoa HOMSO
Mwenyekitik wa Kikundi Mama Mbaruku akitoa Maelezo kwa Wauguzi wa Wodik ya Wazazi katika hospitgali ya mkoa kuhusu sababu ya kutembelea wodi ya Wazazi.
Akina Mama wa Kipare wakionyesha Moyo wao wa huruma ambao Mwenyezi Mungu amemjalia Mwanamke kuwa nik Mtu wa Huruma kwa kutoa Msaada kwa wagonjwa. Hnapo nik baada ya kutoka Wodi za Wazazi ambko walikuwa wakitoa zawadi ya Sabuni kwa wazazi wenzao.
Mama huyo unayemuona ni miongoni mwa wana kikundi cha akina Mama wa Kipare na Walioolewa na Wapare waishio Songea Akiwa katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako wamekuja kutoa sabuni kwa wazazi hapo amepakata mtoto akiwa na Furaha kuzaliwa kwa kuwa siku hiyo ndiyo siku ambayo naye alizaliwa
No comments:
Post a Comment