KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, July 25, 2014

WAVUVI WA MWAMBAO WA ZIWA NYASA WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA VIFAA VYA UWOKOZI NA VIKINGA MAJI ILI KUKABILIANA NA MAJANGA YA KUZAMA ZIWANI DHORUBA INAPO TOKEA

Hiyo ni hali halisi kwa Wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wanavyokabiliana na hali ya Majanga yanayotokea Ziwani, hakuna Uokozi wa uhakika bali kutumia zana za Asili katika kuwaokoa watu wanaopatwa na majanga katika Ziwa Nyasa.
Vijana wa uokoaji katika Mwambao wa Ziwa Nyasa wakitoka kuwaokoa Vijana wawili waliozama kwenye Maji, Yohana Behewa na john Behewa waliozama Kilindini kilometa 20 kutoka nchi kavu katika maeneo ya Kijiji cha Chiulu Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma .
Vijana wa Uokozi wakivuta Mtumbwi uliowaokoa vijana waliokuwa wamezama kutokana na kupigwa na Wimbi wakati wa Dhoruba kali wakati wakiwa Ziwani.
Hapo ni vijana waliookolewa wakiwa wamefikishwa Nchi kavu ambako walipatiwa msaada baada ya kuokolewa na vijana wenzao huku wakiwa wamechoka kutokana na kunywa  maji.
Kikosi cha ukoaji Kilichopo Kijiji cha Chiulu wakivuta mtumbwi uliobeba watu waliowakoa kutoka Ziwani baada ya kupigwa na dhoruba na kuzama majini hali iliyotokana na matumizi ya Zana hafifu ambazo hazikidhi kwa kushindana na Mawimbi makali yanayo tokana baada ya  Dhoruba kali  inapotokea katika Mwambao wa Ziwa Nyasa. Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wamesema hali hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara na hakuna njia nyingine inayotumika kuokoa wahanga wanaopatwa na kadhia hiyo zaidi ya kutumia vifaa duni walivyonavyo.
Mwambao wa Ziwa Nyasa hauna Kikosi cha Polisi cha Wanamaji wa kuweza kusaidia uokozi wa majanga yanayotokea Ziwani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema juhudi za makusudi zinafanywa ili kupata kikosi cha waokoaji wa Maji kwa upande wa Polisi  juhudi zinafanywa ili kupata  kikosi chja wana maji wa Jeshi la Police ,Pamoja na hilo Jeshi la Police litatoa Mafunzo kwa Vijana wanao ishi kandokando mwa Mwambao wa Ziwa Nyasa .

No comments:

Post a Comment