KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, July 20, 2014

RAIS WA JAMUHURI YA TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI RUVUMA



Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa akiwa na Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Alhaji Abdullah  Lutavi wakibadilishana mawazo na Kiongozi mwandamizi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea mwenye Joho Jekundu Mh Charles Mhagama akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho katika Uwanja wa Ndege Ruhuwiko Songea walipokuwa wakisubiri Ujio wa Rais


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Miyayo akiwa na Afisa wa kitengo Maalum wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mkoani Ruvuma Dr. jakaya mrisho Kikwete.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki kushoto Gaudens Kayombo wakipena mawazo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi aliyeshika Bendera akitoa maelekezo kwa Viongozi wa chama juu ya Mapokezi ya Rais muda mfupi kabla ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa wamejipangas mstari kuashiria mapokezi ya Rais aliyekuwa akiwasili uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko.
Wapiganaji wa Serikali ya Jamhurik ya Muungano wa Tganzania wakifuatilia kwa karibu kuingia kwa Ndege ya Rais wa jamri ya Muungano wa Tanzania mh Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Mkoani Ruvuma.
Watumikshi wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula Taifa wakiteta Jambo na Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti katika eneo la Maghala ya Hifadhi ya Chakula lililopo Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula Taifa akifurahia kuona hali ya chakula cha akiba hiyo ni kuonyesha wakulima wanaitika wito wa kulima na kuzalisha kwa wingi na hofu ya uwepo wa njaa haitakuwepo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea akifurahia ujio wa Rais katika kitengo cha Hifadhi ya Chakula ambako kuna mrundikano wa mazao kwani imani yake ni kuwa Rais akishuhudia hali ya Mrundikano ataweza kutoa msukumo wa kupunguza mrundikano ili ununuzi wa mahindi mengine uanze mara moja.


Rais akiwa katika Viwanja vya Hifadhi ya Chakula ambako mahindi yamehifadhiwa kushuhudia mwitikio wa wananchi katika kuzalisha mazao kupitia kilimo.
Msafara wa Rais ukielekea eneo ambako limejengwa Ghala la Chakula lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za Mahindi katika Hifadhi ya Chakula cha akiba ya Ruhuwiko Manikspaa ya Songea.
Ghala lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Ziarani Mkoani Ruvuma ambalo litapunguza kiasi cha tanik 5000 za mahindi ambayo yamekosa hifadhi wakati mengine yakitafutiwa mahali kwa kuyahifadhi ili kupisha nafasik ya kuendelea na ununuzi wa mahindi ya msimu huu. 
Add captionRais wa Jamhurik ya Muungano wa Tanzania akielekea Jukwaani kuongea na wananchi juu ya Ufunguzi wa ununuzi wa Mahindi na namna ya kupunguza mahindi yaliyorundikana katika Hifadhi ya Chakula ya Songea
Rais Jakaya Mriksho Kikwete akisalimikana na Mbunge wa Jimbo la Songea Dr Emmanuel John Nchimbi mara Baada ya Kushuka katika Ndege Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Manikspaa ya Songea.
     Rais akiwa katika eneo la Hifadhi ya Chakula (NMC)akitembelea maghala ya chakula yaliyoko Songea
Rais akiwa kastika kutembelea Mahindi yaliyorundikana katika Hifadhi ya Chakula ya Songea alipokuwa Ziara Mkoani Ruvuma muda mfupi kabla ya kuzindua ghala lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5000 za Mahindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifurahia Akiba iliyopo katika Hifadhi ya Songea.
Rais akiwa katika Hifadhi ya Chakula ya Ruhuwiko, Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma akifurahia uwepo wa Mrundikano wa Tani za Mazao ya Chakula yanayosubiri kutafutiwa hifadhi ili yaweze kununuliwa mengine. Rais amehaidi kuanza ununuzi wa mahindi ya msimu huu tarehe 1/8 /2014 amesema amefanya mazungumzo na Nchi zenye njaa kama Kenya, Sudan Kusini na Shirika la Chakula Duniani ambao watauziwa ili kupunguza mrundikano uliopo  na kupata nafasi ya kuhifadhi mahindi yatakayonunuliwa.
Mh Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete akikagua shehena ya Mahindi yaliyorundikana nje ya Maghala yakisubiri hifadhi ili kupisha nafasi ya kuweza kununua mahindi ya Msimu huu wa 2013/2014
Ghala lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ziara yhake Mkoani Ruvuma ambalo litaweza kuhifadhi kiasi cha Tani 5000 za mazao na kupunguza mrundikano wa mahindi yanayolala nje.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ghala la hifadhi ya Chakula lenyhe uwezo wa kuhifadhi Tani 5000 lililopo katika kitengo cha Hifadhi ya Chakula NMC Ruhuwiko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za NHC za gharama nafuu zilizopo Mkuzo Manispaa ya Songea utagharimu kiasi cha Shilingi 676,244,201  zitakazotumika kujenga Nyumba 18 ambazo zitauzwa kwa wananchi kwa shilingi milioni 36.3 hadi Milioni 44.4. Zinazoonekana pichani ni Nyumba zinazojengwa Mkuzo ambazo Mh Rais amezindua ujenzi wake.
Waandishi wa Habari wakiwa kazini kupata matukio ya Zikara ya Rfais wa Jamhuri ya Muungano wa Tganzania akiwa Mkoani Ruvuma Manispaa ya Songea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi katika viwanja vya Ofiksi za PCCB baada ya uzinduzi wa Ofisi hizo.
Watumishi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa Ziara Mkoani Ruvuma, Hapo ni mbele ya Jengo la Ofiksi za PCCB muda mfupi baada ya kulizindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Watumishi wa Taasisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma mbele ya Jengo la Ofisi za TAKUKURU mkoanik Ruvuma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma akisalimikana na Mwandishi mwandamizi wa Uhuru Fm na Mwariri Mwandamizi wa Rural Press Juma Nyumayo, wa katikati ni mwandishi wa Star TV na mmiliki wa Blog ya Songea Habari Bw. Adam Nindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meneja wa Hifadhi ya Chakula wa Mkoa wa Ruvuma Mogan na wafanyakazi wa Kitengo Wakala wa chakula Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kuwasili Kitengo cha Hifadhi ya Chakula cha Songea.
Wanafunzi wa Club za Wapinga Rushwa wakiwa katika Picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na kushoto  baada ya Rais na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bi Mary Mosha, anayefuata ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Mbunge wa Jimbo la Songea Dr Emmanue Nchimbi akiteta na Waziri wa Ujenzi akimshauri kuhusu kuangalia uwezekano wa kukamilisha ujenzi wa Barabara za Lami za Manispaa ya Songea.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dr. Emmanuel John Nchimbi akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi kabla ya kuwasili Rais katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko, Manispaa ya Songea.
Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli wa kwanza kushoto, akiwa na mwaandishi wa Chanel Ten Emmanuel Msigwa na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dr. Emmanuel John Nchimbi wakiwa Uwanja wa Ndege Ruhuwiko wakisubiri ujio wa Rais wa Jamuhuri yaMungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete .
Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Ruvuma Mihayo akiwa na Mwandishi wa Habari wa Star Tv, Adamu Mzuza Nindi  na Viongozi  wa Mkoa wa Ruvuma wakibadilishana mawazo wakati wakisubiri kumpokea Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete  katika uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko, Songea.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiwa na wakuu wa mikoa wenzake katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Songea wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDr Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anawasili katika  Ziara Mkoani Ruvuma. kutoka kushotoMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu aliye katikati ni   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama na kulia aliyeshika handbag ni mkuu wa Mkoa wa Katavi Inginia Stela Manyanya.
Waalikwa mbalimbali waliokuja kuhuduria Uzinduzi wa Jengo la Ofisi za PCB Mkoa wa Ruvuma
Watumishi wa TAKUKURU wakiwa katika Maadhimisho ya Uzinduzi wa Ofisi za TAKUKURU za Mkoa wa Ruvuma. Hapo wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa PCB Mkoa wa Ruvuma akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi  TAKUKURU Taifa Mary Mosha  ili aweze kutoa taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Taasisi hiyo na kuelezea hali ya Rushwa kwa Mheshimiwa Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa Hotuba katika Viwanja vya Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma muda mfupi baada ya kulizindua Jengo hilo. Rais amewataka Maafisa wa TAKUKURU kuwa wasiri na taarifa zinazotolewa na Wananchi kuhusu vitendo vya Rushwa ili waweze kufanikiwa katika kutokomeza Rushwa.
Pichani ni Jengo la Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lililozinduliwa na Mh Rais wa Jamri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Jengo hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1,189,708,769.70
Viongozi mbalimbali na wafanya kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma waliokuja kuhudhuria Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli akiwa na Mwandishi mwandamizi wa Radio Free na Star TV Songea Adam Nindi katika viwanja vya Ofisi za PCCB Mkoa wa Ruvuma muda mfupi baada ya Uzinduzi wa Jengo hilo lililopo Kata ya Mahenge Manispaa ya Songea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mbele ya Jengo la Ofisi za Taasisi hiyo alilolizindua akiwa Ziarani Mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment