Waislamu Mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa na umoja na kufuata
Mambo mazuri ambayo hayawezi kuiweka Nchi Mahali pabaya, Umoja Mshikamano na
kuaminiana ndiyo silaha ya kuweza kuendeleza Amani.
Mataifa ya Waarabu yameingia katika Vita na kukosa Amani
kutokana na Unafiki na kuyajali Mataifa makubwa. Hayo yamesemwa katika
kusherehekea Sikukuu ya Iddi Fitri Mjini Songea.
Sheikh Shaban Chitete wa Masijidi Huda
amesema endapo Waislamu watakuwa wanafiki basi huo ndio utakuwa mwanya wa watu
wabaya kupata nafasi ya kuwagombanisha, amesema katika kuitafuta Katiba Mpya
Wabunge tuliowachagua wamejigawa na kujiita Ukawa hiyo ni kutaka kufuja Fedha
za Wananchi .
Waumini wa Dini ya kiislam Katika
Misikiti mbalimbali ya Manispaa ya Songea wamemuomba Mungu aendekeze Amani na
Utulivu tulionao na kuwaombea wale wenye nia ya kutaka Taifa la Tanzania
liwe na Mfarakano washindwe. Alahamdulilahi Labiramina,
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Ruvuma Mauridi Hassan Said
ameiomba Serikali kuangalia upya kuhusu Ujenzi wa Mabucha ya Nguruwe, kuweka Mabucha
ya Nguruwe hadharani kama ilivyo katika Soko
la Mazao SODECO ni kuwadhalilisha Waislam. Waislamu wanashindwa kununua bidhaa
katika Soko la SODECO kutokana na Mabucha ya Nguruwe kuwa wazi wazi.
Sheikh Shabani Chitete akiwa katika membali ya Masijid Huda Mabatini akitoa Hotuba ya Sikukuu ya Iddi FitiriMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka Waislamu kuwaimarisha watoto katika kujiendeleza kielimu
Katibu wa BAKWATA amesema katika kuendeleza Elimu kila
Msikiti utakuwa na Shamba la zao la chakula, pia kila Msikiti utakuwa na Orodha
ya Waislam na orodha zao kila msikiti uhakikishe una ekari mbili za miti ili
kulinda mazingira.
Wanafunzi wa Shule ya wasichana Songea wakiwa nje ya Msikiti wa Masijidi Huda wakifurahia Iddi FitiriMzee na Familia yake wakitoka kuswali katika msikiti wa Huda Mabatini Manspaa ya Songea
swala ya iddi firiri
Iddi Mbara kwa waislamu, wahimizwa kuwa na upendo wenyewe kwa wenyewe
waumini wa msikiti wa mjini kati wakiwa katika dua la kupombea amani Serekari ya Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika Baraza la Iddi lililofanyika katika
ukumbi wa Songea girls. Amesema Waislamu ili kuyafikia Maendeleo ya kweli ni
lazima wajidhatiti katika Elimu hasa kwa kuwaendeleza watoto wao.
Masijidi Huda katika Manisipaa ya Songea waumini wakiwa ndani ya Msikiti
Hivyo hivyo wanaume walio kosa nafasi ndani ya Msikiti wakiwa wana swali nje ya Msikiti wa Mjini kati Songea
Akina mama katika Msikiti wa Mjini Kati katika Manispaa ya Songea wakiwa wametandika Mikeka Nje baada ya kukosa nafasi ndani ya Msikiti
wanawake wakiwa msikiti wa mjini kati songea
Akina mama walio miminika katika Msikiti wa Masijidi Huda wakiwa Tayari kwa Swala ya Iddi
Aidha Katibu wa BAKWATA Maurid Hassan Said amesema Waislamu
walio wengi ni wakulima, mwaka huu kumekuwa na Mahindi mengi. Mwaka jana
Serikali ilinunua Tani 53,000 tu za mahindi. Mwaka huu Inatarajia kununua Tani
48,000 Nipungufu kuliko mwaka jana
katika ununuzi. Wameiomba Serikali kuongeza ununuzi ili kuwaokoa Wananchi
katika kukabiliana na Umaskini.
Waisilamu Katika Manspaa ya Songea Wakiombea Amani wakati wa Swala ya IddiWaisilamu wakiwa katika swala ya iddi katika msikiti wa Huda Mabatini mjini Songea
No comments:
Post a Comment