Mgombea Udiwani Kata ya
Msamala wilayani Songea Isaack Lutengano akiwa kwenye Kampeni kwa kutumia
Mabango ya Vivesheo vya Tayari.
Wagombea kupitia Chama cha Mapinduzi Mkoani
Ruvuma wametakiwa kuchagua Viongozi ambao wataleta Maendeleo na siyo
kuchagua Kiongozi kwa sababu ya Umarufu
wa Jina.
Mgombea Udiwani Kata ya Msamala kupitia Chama cha
Mapinduzi CCM Isaack Lutengano amesema
vijana walio wengi wapo katika mpango wa kutaka Mabadiliko lakini lazima wawe
makini katika Mabadiliko hayo, wasichague Viongozi ambao hapo baadaye
watajijutia. La msingi ni wao Vijana kuangalia Viongozi watakao ondoa Kero zao.
Mjumbe wa kamati ya Siasa
Wilaya ya Songea OSAMU ULAYA akiwa na Bango la Mgombea Udiwani Kwa tiketi ya
CCM wa Kata ya Msamala.
Wanachama wa CCM
wakiunganisha nguvu kwa ajili ya Ushindi hapo Oktoba 25.
Mjumbe wa kamati ya Siasa
Wilaya ya Songea OSAMU ULAYA akiwa na Bango la Mgombea Udiwani Kwa tiketi ya
CCM wa Kata ya Msamala.
Mke wa Mgombea Udiwani Shada
Haule akiomba kura kwa wajumbe kwa ajili ya Mumewe.
Mgombea udiwani Kata ya msamala Isaack Lutengano
akipata usingizi baada ya kukesha kufanya kampeni za Uzinduzi Rasmi wa kuanza
kampeni
Mgombea Udiwani kwa Tiketi ya
chama cha Mapinduzi Kata ya Msamala Manispaa ya Songea akihutubia wananchi
jinsi atakavyoendeleza Kata ya Msamala ikiwa ni pamoja na Kufungua Saccos,
Vituo vya Mafuta na kuunda Vikundi mbalimbali.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya
Msamala Filipo Shemtembo akizindua Kampeni Kata ya Msamala.
Akina Mama wakisikiliza Sera
mbalimbali kutoka kwa Wagombea wakati wa Ufunguzi wa Kampeni.
Madiwani watarajiwa wa Viti
Maaluma Kata ya Msamala Asia Chakwela na Hapiness Haule wakiwa wamepiga magoti
huku wakiomba wafanikiwe ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Akina Mama wakisikiliza Sera
mbalimbali kutoka kwa Wagombea wakati wa Ufunguzi wa Kampeni.
No comments:
Post a Comment