Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akiwa na Kamati ya Usalama Barabarani wakitoa elimu ya usalama Barabarani kwa watumiaji wa Barabara. Amewataka Madereva wa Pikipiki kuzingatia usalama wao kwanza kwa kuzingatia sheria zilizowekwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Captn Mstaafu Filipo Shemtembo.
Mtoa Elimu ya Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Zuberi Muya akiwasisiza Madereva wa Pikipiki kujisajili katika vijiwe vyao na kutowakimbia askari wanapowasimamisha, kufanya hivyo kunawasaidia kujiepusha na ajali na matatizo yanayowakuta ikiwa ni pamoja na kunyang`anywa pikipiki na kuuwawa. Amewashauri kutoa taarifa kwa wenzao wanapokodiwa na watu wasiowafahamu hasa nyakati za usiku au katika maeneo hatarishi.aliye kulia ni Asikari wa Usalama Barabarani Joseph Lukasi Shimba
Madereva wa Pikipiki maarufu kama yeboyebo wa Manispaa ya Songea wakisikiliza Elimu ya Usalama Barabarani iliyotolewa wiki ya usalama barabarani katika vijiwe vya waendesha pikipiki vya Mshangano Stend, Soko Kuu na Lizaboni stend wakati wa uzinduzi wa wiki ya Usalama Barabarani Mkoani Ruvuma.
Kamada wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amewataka Madereva Mkoani Ruvuma kutoa taarifa za kuashiria kutendewa uhalifu pindi zinapotokea kwa kumpigia simu au kumbip au kutuma ujumbe wa tafadhali nipigie ili kupewa msaada na Jeshi la Polisi. Amesema simu ya Ofisi ipo kwa ajili ya kuhudumia wananchi pindi wanapotendewa uhalifu au kumtilia mashaka ya uhalifu mahali fulani.
Madereva wa Pikipiki na Magari waliokuwa wakipokea Elimu ya Usalama Barabarani wameliomba Jeshi la Polisi kutumia busara wanapowakamata madereva kwa makosa ya barabarani wasifanye kama wana uhasama na madereva wa Pikipiki hali hiyo inawafanya madereva wa Bodaboda kutojiamini pindi wanapokutana na Askari na kuwakimbia kwa kuona ni adui kwao. Aidha wameomba Elimu ya Usalama Barabarani iwe inatolewa mara kwa mara ili kukumbushana isisubiriwe wiki ya usama barabarani pekee kwa kuwa watumiaji wa vyombo vya moto wanaongezeka siku hadi siku ambao wanahitaji Elimu.
No comments:
Post a Comment