Kati ya Nchi 22 za
Afrika Tanzania imepata
faida baada ya kupata ufadhili wa kupata Elimu ya Kilimo Hifadhi Kutoka AGRA
[Nyota ya kijani ]na kuwafanya Wakulima kuongeza kipato cha mavuno kutoka gunia 4 hadi Gunia 28 kwa
Ekari.
Katibu Mtendaji Mkuu kutoka ACT
Saidi Mkomwa amesema jumla ya wakulima
100,000 kutoka Bara la Afrika wamepata
Elimu ya Kilimo Hifadhi jambo lililosababisha ongezeko la mavuno na kuifanya AGRA kuwajibika kutafuta
masoko kwa mazao yanayozalishwa Afrika.
Afisa Mtendaji wa Kilimo Hifadhi kutoka Kenya Saidi Mkomwa amesema
juhudi zinazofanywa hivi sasa na ATC ni kuhakikisha wakulima waliopewa Elimu ya
Kilimo Hifadhi wanakuwa walimu kwa wakulima wenzao ili kasi ya uzalisha na
kuondoa umasikini miongoni mwawananchi uwe mkubwa.
Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la ACT Kutoka Kenya Saidi Mkomwa amesema hayo wakati
wa mafunzo kwa wakulima 50 kutoka mikoa ya Ruvuma,Iringa na Njombe amesema Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa Ardhi
kwani nao wawekezaji wa Kilimo wanajivunia Hekta 1,000,000 za Ardhi za Kilimo Hifadhi,
hivyo vijana hawana haja ya kukimbilia Ulaya wakiuacha utajiri Nchini mwao.
Wakulima kutoka nyanda za juu kusi wakiwa katika mjadala mkoani Njombe katika ukumbi wa fm
Katika Nchi 22 za Bara la Afrika zinazo fadhiliwa na AGRA, katika Kilimo
Hifadhi kazi kubwa iliyo baki ni kuwakopesha wakulima vifaa vya kisasa,
pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za fedha
ili waweze kupata mikopo.alimaliza
katibu saidi Mkomwa
Wakulima wakiwa katika majaribio kuzijua dawa mbalimbali za kilimo huku wakisikiliza kwa makini matumizi halisi ya Pembejeo
Mtaalamu wa Kilimo Kanda ya Kusini Abiudi Gamba amesema
anajivunia Elimu ya Kilimo Hifadhi kwa kuwa Wakulima kutoka wilaya za Ludewa,
njombe, Songea Vijijini na Namtumbo wamekuwa wataalamu katika Kilimo, Naye Mkulima
Kutoka Kijiji cha Namatuhi Songea Vijijini Winiley Nindi amesema kutokana na
utaalamu alioupata katika Mafunzo ya siku nne kutoka ACT utamwezesha kuongeza mapato zaidi.
Katika Nchi 22 za Bara la Afrika zinazo fadhiliwa na AGRA, katika Kilimo
Hifadhi kazi kubwa iliyo baki ni kuwakopesha wakulima vifaa vya kisasa,
pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za fedha
ili waweze kupata mikopo.alimaliza
katibu saidi Mkomwa
No comments:
Post a Comment