Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema ili kuimarisha uchumi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa Serikali imeamua kujenga karakana ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza Boti kubwa na ndogo
Wilaya y Nyasa ina Vitega Uchumi vingi ikiwemo Mali asili kama
Milima ya Living Stone, Ufukwe wa Ziwa Nyasa, Samaki wa Mapambo, pamoja na
visiwa ambavyo vinaweza kuwa vyanzo vya Utalii.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Neema Malenga akiwa na Mwandishi wa Habari Judith Lugoye wakiwa mwambao wa Ziwa nyasa
Njini ya ya Mitumbwi ni hizo kafia alizo chukua huyo kijana ambapo kama huja shiba huwezi kuendesha mtumbwi
Vifaa duni vinavyo tumika katika kuvulia Samaki katika Ziwa nyasa hapo Vijana wanatoa mtumbwi tayari kwenda kuvua
Pamoja na utengenezaji wa Zana za kisasa Wananchi wa Kijiji
cha Chiulu wameiomba Serikali kutazama upya samaki waliopo katika Ziwa Nyasa,
wapo samaki ambao hawakui ambao ni pamoja na Vituhi, Unjukwa, ambao hata
ukiwapasua utawakuta wakiwa na mayai, hali hiyo ni kuonyesha kuwa hawezi kukua
tena, kukataza kuwavua ni kurudisha nyuma uchumi wa wananachi wanaoishi kando
kando ya Ziwa Nyasa.
Hebu ona mtubwi ulivyo nesa kwa nyuma huku maji yakiingia hilo ni jambo la kawaida kwa wavuvi
Ndugu yangu usikie kitu kinacho itwa mutumbwi ukingia kama una BP basi ujue kila wakati roho ita kuwa juu hebu ona hawo vijana wakiwa katikati ya ziwa
Wavuvi wa Ziwa nysaa wakijiandaa kwenda kuvua samaki kilometa hamusini kutoka nchi kavu
Mwambao wa Ziwa Nyasa
Moja ya samaki wanao patikana katika Ziwa Nyasa hao ni Mbufu na Kambare
Jambo mhimu ni wewe msomaji kuji sogeza Mwambao wa Ziwa Nyasa ili ukajionee jinsi samaki hawa unao waona walivyo watamu
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akiwa amekaa kando kando ya Ziwa
Nyasa kutathmini Maendeleo ya Wilaya ya Nyasa yanavyosonga mbele.
Unavyo sikia swala la Utalili ni pamoja na viongozi kutembelea ufukwe wa ziwa nyasa na kuona uwekezaji uanao fanywa na watu mbambali hapo Mkuu waWilaya ya Nyasa akikagua Maeneo sehemu ya Bio Camp Lodge iliyoko Mbambabay
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akiwa Bio Camp Lodge akipunga upepo
kuonyesha mfano kwa watu wengine katika kudumisha utalii wa ndani kwa
kutembelea vivutio vyetu.
Hii nimoja ya karakana ya kutengenezea Maboti ya kisasa ambayo ime gh'arimiwa na Serekari ya Tanzania kwa kutoa shilingi milioni
Bio Camp Lodge Mbambaba Nyasa
Bio Camp Lodge Mbambaba Nyasa
Bio Camp Lodge Mbambaba Nyasa
Bio Camp Lodge
Pamoja na kuimarisha uchumi wa Wananchi wa Mwambao wa Ziwa
Nyasa wanahitaji Vitega Uchumi, hapo ni uwekezaji mkubwa wa nyumba za kulala
wageni zilizojengwa na Watawa wa kike Masista wa Shirika la Mtakatifu Vicent
juu ya Mlima wa Mbamba Bay.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema pamoja na ujenzi huo Serikali
inatayarisha majokofu ili wavuvi wawe na sehemu ya kuweka Samaki waliovuliwa
lwakati wakisubiri bei nzuri kuliko kuwasukuma kwa bei ndogo.
Wavvi katika Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema pamoja na kukosa
Samaki lakini changamoto nyingine ni pamoja na kukabili kuchomewa Nyavu mara
kwa mara.na Afisa Uvuvi wakidai kuwa ni nyavu ndogo jambo
linalosababisha kuwaacha wavuvi katika hali ya umaskini.
Wananchi wa Mwambao
wa Ziwa Nyasa wilayani Nyasa wameiomba Serikali kuwasaidia Zana Bora za Uvuvi
ili kusaidia na kuepusha vifo vinavyotokea baada ya kukosa Zana Bora.
Wananchi hao wameyasema hayo wakati
walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari kuhusu kuporomoka kwa uvuvi katika
Ziwa Nyasa kwa kupata Tani moja za Samaki wakati walikuwa na uwezo wa kupata
Tani zaidi ya tatu.
Karakana ya Kutengeneza Boti za Kisasa imejianda kwa kuweza kununua Genereta za kuweza kusaidia endapo umeme uta katika
Hiyo ni garama ya Vitu utakavyo taka kuvitumia hapo Bio Camp kwa kweli pame pendeza Bio Camp Lodge
Vitega Uchumi kwa ajili ya Watalii, Nyumba unazoziona hapo
ni Nyumba za kulala wageni ambazo zinajulikana kwa jina la Bio Camp Lodge Mbamba Bay
yenye vyumba zaidi ya 40 na maeneo mengi ya kupumzika na kuburudika na michezo
mbalimbali ikiwemo na ngoma za asili.
Bio Camp LodgeUmeme unao tumika hapa unategemea Kinyesi cha Wanyama hivyo umeme haukatiki muda wote njoo uone Bayo Gess inavvyo fanya kazi
Picha hizo zote ni kukufanya Msomaji uone hali halisi ya Bio Camo Mbambabay
Uezekaji wa Nyumba hizi ume tumika zaidi Nyasi hivyo pamoja Wilaya ya Nyasa kuna Joto lakini eneo hili ni Baridi kwenda Mbele kwa kweli Mbambabay Imependeza
Mwandishi wa Habari Judith Lugoye ambaye aliweza kubahatika kulala hapo amesema ukilala hapo ndoto unazo ota ni za kimaendeleo tu utajiri una kuwa mikononi mwako
Nyumba vilivyopo vina jitegemea kila nyumba ni chumba kimoja ,hiyo nihali halisi ya Bio Camp
Bio Camp ina jali afya za wateja wake chandarua unacho kiona mbuu akisogea mita moja tu kutoka kwenye chandarua basi ujue mauti yata mkuta hayo yote yanafanywa kulinda afya ya mteja
Mambo haya tulizoa kuya ona Ulaya lakini kitanda unacho kiona kipo Mbambabay kwenye Bio Camp ukifika huko utaona vitu tofauti na jinsi unavyo fikili maendeleo yaliyoko ni kama miujiza
Utalii unanda na Familia hapo Mkurugenzi wa Bio Camp akiwa na familia yake kuangalia Maadhari ya Camp hiyo
Pamoja na Kuangalia Maendeleo ya wilaya ya Nyasa ni pamoja na kuhusisha wagombea wa kisiasa ona walio gombea majina yamepagwa kutokana na matokeo ya kura za maoni
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema pamoja na ujenzi huo Serikali
inatayarisha majokofu ili wavuvi wawe na sehemu ya kuweka Samaki waliovuliwa
lwakati wakisubiri bei nzuri kuliko kuwasukuma kwa bei ndogo.
No comments:
Post a Comment