Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrew Kuchonjoma amewataka
waandishi wa Habari kuwa na umoja katika mambo mbalimbali, pia amewataka
Waandishi kujiendeleza katika Elimu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma
(RPC) Andrew Chatwanga amewataka Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuimarisha
Vitega Uchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Redio pamoja na kujenga Ofisi na
Nyumba za kulala wageni. Mradi wa Redio mpaka kukamilika unahitaji shilingi
Milioni 25.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa
Ruvuma, Ngaiwona Nkondora ameombwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa
Habari Mkoa wa Ruvuma kuwa mvumilivu na mtulivu katika kutekeleza masuala ya
klabu ya waandishi wa habari wa Ruvuma Press Club (RPC)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Marietha Msembele amewataka waandishi wa habari
kushirikiana naye katika Uongozi, hakuna kitu ambacho kiongozi peke yake
anajua.
Mweka hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa
wa Ruvuma Alpius Mchucha ameomba kupewa ushirikiano na waandishi katika
kutekeleza majukumu yake.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Ruvuma
Press Club wametakiwa kuwasukuma Viongozi wa ngazi za juu ili walete Maendeleo
ndani ya Chama cha Waandishi wa habari.
Wajumbe waliochaguliwa katika Kamati ya Utendaji ni, Kassian Nyandindi, Mpenda Mvula,Geofrey Nilahi, Joseph Mwambije na
Mpenda Mvula kiongozi wa Kamati ya Utendaji sijui ana fikilia kupiga Mzinga Gani bora afikili e Maendeleo
Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi
wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani
Ruvuma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ruvuma Press Club wakiwa na Furaha baada ya kuwapata Viongozi
Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi
wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani
Ruvuma.
Mwandishi Andrew Mwaiki akiwa kwenye uchaguzi jengo la ushirika songea
Mwandishi Cerencesia Kapinga ambaye alikuwa katika kamati ya Utendaji kwa hivi sasa hakugombea kutokana na Jukumu la kugombea kata ya Ndirima Litembo hapo October 25 Mwaka huu
No comments:
Post a Comment