KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, October 7, 2015

JENISTA NA MRADI WA MAJI JIMBO LA PERAMIHO SONGEA VIJIJINI ATUMIA SHILINGI MILIONI MIA MOJA THEMANINI


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peramiho kupitia Chama cha Mapinduzi Jenista Johakimu Mhagama ameomba kuchaguliwa tena ili aweze kumaliza Miradi ya Maji na Miundo mbinu ya Barabara aliyoianza.


Mheshimiwa Jenista Johakimu Mhagama mpaka sasa kwa mradi wa Maji ameshatumia kiasi cha Shilingi Milioni 180 kwa kutandaza Mabomba na kujenga matangi ya Maji.

Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Jenista Mhagama amesema kazi iliyobaki kwa Upande wa Maji ni kuingiza Maji kwenye Tanki na kusafisha Mabomba ili maji yaweze kuanza kutumika
 Watanzania Mwaka huu wamekuwa makini na kampeni wana sikiliza kwa makini ili October wasifanye makosa

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewaomba wagombea wote wa vyama vya upinzani kufanya kampeni kwa Amani na Utulivu pia kuachana na kuweka mabango katika sehemu hatarishi kama kwenye nguzo za umeme

 Wananchi wakisikiliza sera mbalimbali kutoka kwa wagombea katika kijiji cha Matimila songea vijijini

Mwenyekiti wa kampeni Jimbo la Peramiho Jumanne Nyingo amewaomba Wananchi kuacha kujiingiza kwenye vyama vinavyoendeshwa kiundugu.Naye Mgombea Udiwani kata ya Matimila Menasi Komba ameainisha shuguli zilizo fanyika na na ccm

Wapiga kampeni wa Mgombea Uchaguzi Jimbo la Peramiho wakipiga Baragumu ya Pembe3 ya Ng'ombe wakati wa Kampeni

No comments:

Post a Comment