Wananchi wa mkoa wa Ruvuma wameshukuru kuona Uchaguzi wa Mwaka 2015 umekuwa
wa Amani na Haki mbali ya Changamoto ndogo
ndogo zilizojitokeza.
Wananchi hao wakitoa Maoni yao katika Maeneo mbalimbali wamesema walichokitegemea
siyo kama ilivyotokea, wakiongozwa na
Emanuel Msabila ambaye aligombea Ubunge
Jimbo la Songea Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo amesema wat wanaogombea
ni lazima ujue kuwa katika kuchaguliwa kuna kushindwa na kushinda mtu
anayeng`ang`aniza kushinda ujue mtu huyo hajui mabadiliko. Akieleza upande wake
amesema unapogombea kuna vitu viwili kushinda na kujenga jina . Mimi Msabila
emanuel Msabila nashukuru nimejenga jina.
Mgombea Ubunge jimbo la Nyasa Inginia Stela Manyanya akiwa katika Furaha Mara Baada ya Kutangazwa kuwa Mshindi Kushoto kwake ni ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Magret Malenga
Jimbo la Songea Mjini katika nafasi za Udiwani CCM imeweza
kuchukua kata 16 kati ya kata 21 za jimbo la songea na Viti 5 kuchukuliwa na
Upinzani.
Msimamizi wa Jimbo la Songea Rafael Kimari amezitaja
kata zilizochukuliwa na Upinzani kuwa ni kata za Matarawe, Mfaranyaki, Ruvuma, Shule ya Tanga na Kata ya Matogoro iliyochukuliwa
na Chama cha CUF. Kata ya Matogoro ndiyo
iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama
Mgombea Ubunge wa Viti Maalu kupitia CCM Mkoa wa Rvuma Jackline Msongozi amesema yeye
kipao mbeleb ameweka kutetea haki ya mama na Mtoto katika kuzuia ukatili wa
kijinsia pia kulinda haki za Wazee naye Diwani wa Kata ya Msamala Manspaa ya Songea Isack Lutengano wamesema
swala lake la kwanza ni kusimamia mindo mbinu ya barabara bila kujali itikadi
za chama
Hali ilivyo kuwa Wakati wa Kupiga kura Katika Jimbo la Nyasa wakiwa katika Mstari majira ya Saa kumi na Mbili Alufajiri
Wanchi wa Mkoaq wa Ruvuma wakipitia Maqgazeti mbalimbali kuona hali ya Matokeo Sehemu Mbalimbali
Wasimamizi wa Uchaguzi katika Vituo mbalimbali wakiongozwa
na Hela Mayao wameiomba Serikali upande
wa Wasimamizi wa Uchaguzi katika Vituo mbalimbali kuandaa Mpango wa kuweza
kupata Chakula kwa kuwa wakiingia katika Vituo hawana nafasi ya kutoka kutafuta
Chakula, jambo linalowaweka kwa muda wa masaa 36 kukaa bila kula hadi
wanaporudi Nyumbani.
Watazamaji kutoka Nchi za Ulaya wakiangali jinsi wasimamizi wa Uchaguzi wakiunganisha Matokeo kwa Njia ya Mtandao
Wasimamizi kutoka Nchi za Ulaya wakiongozwa na Msimamizi
msaidizi Nansi Nansi kuwa kwa hatua ya kupiga mpaka kuhesabu kura uchaguzi
umekuwa wa Uhuru na Amani. Amewataka watanzania kuwa na Amani.
Watazamaji wa
Kimataifa kutoka Nchi za Ulaya Nansi Nansi wamesema uchaguzi wa Mwaka 2015
umekuwa wa Haki na Amani.
Msimamizi Msaidizi wa
kimataifa kutoka Nchi za Ulaya Nansi Nansi amesema ingawa bado tukiendelea
kungoja Matokeo ya Urais kutangazwa lakini mpaka hapa tlipofikia panaonyesha
Hali ya Amani
Uchaguzi katika Jimbo la Songea ulikabiliwa na Changamoto ya
Wanachama wa CHADEMA kugomea Matokeo na kufanya Maandamano yasiyo na kibali na
kuwalazimu Jeshi la Police kutumia Mabomu ya Machozi kutawanya Waandamanaji.
Anna Tembo Mtetezi katika Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma akiwa katika ulinzi kutetea Haki ya Mama na Mtoto
Kaimu Mkurugenzi wa Jimbo la Songea Rafael Kimari amesema kati ya
Wagombea watatu walioshiriki katika Uchaguzi nafasi ya Ubunge akiwemo manuel
Msabila wa ACT, Joeph Fyime wa CHADEMA na Leonidas Gama wa CCM .
Akisoma Matokeo ya Uchaguzi nafasi ya Ubunge Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Rafael Kimari alisoma kura alizopata kila
mgombea Emanuel Msabila kutoka ACT ALIPTA KURA 436 , Joseph fyime wa chadema 37, 012 na Leonidas gama wa CCM KURA
40,886
Kaimu Mkurugenzi Wa Manspaa ya Songea Raphael Kimary akipata Tarifa kutoka sehem u Malimbali
Wananchi waliohojiwa na Star TV wamesema Uchaguzi ulikuwa
Uhuru na Amani, ila sheria ya kukaa mita 200 inatakiwa ifanyiwe upembuzi
yakinifu, nao wasimamizi wa Uchaguzi wameomba serekari kuweka mpango malumu kwa wasimamizi
kupewa chakula kwa kuwa muda wa kwenda kula una kuwa haupo baada yake hushinda
njaa kwa masaa 36 hadi wanapo rurudi nyumbani sik ya pili
Mgombea Ubunge Jimbo la Songea Mjini kwa tiketi ya CCM
Leonidas Gama mara baada ya kutangazwa
kuwa Mbunge amesema yeye kama Mbunge wa Jimbo
la Songea ana wahakikishia wananchi wote kuwa atafanya kazi kwa niaba ya Vyama
vyote ili kuleta Maendeleo katika jimbo la Songea.
Hadi Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Songea Rafael Kimari Akimtangaza Mgombea Ubunge kwa
tiketi ya CCM Leonidas Twitbet Gama kushinda kwa kura Dhidi ya Mgombea wa CHADEMA Joseph Fyime
aliyepata kura na Mgombea wa ACT
Wazalendo Emanuel Msabila aliyepata kura.
Wafuasi wa CHADEMA wametakiwa kuwa na watulivu wakati wote
wa kutolewa kwa Matokeo, Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Police Mkoa wa
Ruvuma Mihayo Msikhela baada ya Wafuasi wa CHADEMA kupokea Taarifa ya kuwa
Mgombea wao wa Ubunge Jimbo la Songea Joseph Fuime ameshinda kauli ambayo
ilileta Mtafaruku.
Wananchi waliopiga kura wakiongozwa na Eliasi Ndimbo
wamesema Wabunge watakapoketi katika kutunga Sheria waangalie Sheria ya
uchaguzi inayowataka kukaa mita 200 irekebishwe ili kuipa nafasi ya kuangalia
kwa ukaribu kinachoendelea katika Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment