Wafiwa na wafasi wa UKAWA wakiwa na simanzi kwa kupoteza mwenzao ERASMO NYINDI
Mh Wiloni akiwa na Viongozi wa Kanda wa UKAWA katika Msiba wa Mhamasishaji Erasmo Nyindi uliotokea Mkoani Ruvuma
Wafuasi wa Ukawa Wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mpendwa wao Erasmo Nyindi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mbeya.
Wanachama wa Mkoa wa Ruvuma wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Erasmo kiongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Waombolezaji wakimlilia mpendwa wao
Maandalizi ya Safari ya Mwisho ya Marehemu Erasmo yakifanywa na viongozi m,balimbali wa UKAWA katika Eneo la Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
Gari iliyosafirisha mwili wa Marehemu Erasmo Nyindi kutoka Songea mkoani Ruvuma kuelekea Mbeya.
Mwili wa Marehemu Erasmo ukitolewa kwenye Chumba cha kuhifadhi Maiti kupeleka kwenye gari tayari kwa kuanza msafara wa kuusindikiza nyumbani kwao mbea.
Waombolezaji wakiomboleza msiba wa Erasmo Nyindi katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma iliyopo Manispaa ya Songea.
Viongozi
wa Chadema wana fanya Taratibu za kusafirisha Mwili wa Marehemu Mhamasishaji
Erasmo Nyindi kwenda nyumbani kwao mkoa wa Mbeya kwa mazishi bwana ametoa
na bwana ame twaa jina lake lihimidiwe, amina.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa CHADEMA wakibadilishana mawazo juu ya Tanzia ya msiba walioupata.
Viongozi a CHADEMA wakiwa katika hali ya majonzi na kushindwa kuamini kilichotokea kwa mpenda wao.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi amesema kifo hicho kimetokana
na Ajali ya Gari lenye namba za usajili T. 501 BBX aina ya Noah iliyotokea
katika eneo kijiji cha Chunya wilayani Mbinga, na uchunguzi bado unaendelea.
Waombolezaji na wafuasi wa UKAWA Mkoani Ruvuma wakiwa viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa.
Wanachama na Viongozi wa UKAWA waliokusanyika nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ili kufanikisha mipango ya kusafirisha mwili wa Mpendwa wao Erasmo Nyindi aliyefariki dunia wilayani Nyasa kwa ajali ya Gari iliyotokea usiku wa tar 2/10/2015
Wanachama wa CHEDEMA wakiingiza kwenye Gari Jeneza la Erasmo Nyindi tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Mkoani Mbeya kwa Mazishi.
Baadhi ya Wafuasi wa UKAWA waliokuwapo Katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kuuaga mwili wa Marehemu Erasmo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mbozi Mkoani Mbeya kwenye Makazi yake ya Milele.
Waombolezaji wakiwa katika hali ya mshangao na majonzi kwa kuondokewa na kada wao.
Waombolezaji ambao pia ni wanachama wa CHADEMA wakiomboleza katika Msiba wa kada wao Erasmo Nyindi katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO)
Waombolezaji wakimwimbia nyimbo za buriani Marehemu Erasmo Nyindi.
Jeneza la mpambanaji na mhamasishaji wa Kampeni za Uchaguzi kupitia UKAWA kanda ya Nyanda za juu Kusini Erasmo Nyindi likiingizwa kwenye Gari tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Nyumbani kwao Mkoani Mbeya.
Wafuasi wa UKAWA wamesema wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mtu wao muhimu katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Wamesema amekufa kishujaa akiwa kazini kutekeleza majukumu yake ya kupigania ushindi wa Ukawa Daima atakumbukwa kwa kazi zake na mchango wake ndani ya chama.
Mtendaji
Mkuu wa Kampeni za Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Rajabu Kaluwa amesema
ajali hiyo ilisababishwa na watu walioshika tochi nyakati za usiku wakiwa na
silaha kutaka kuteka nyara msafara wa Mgombea Ubunge katika Jimbo la Nyasa Bw.
Cathbet Saule almaarufu kwa jina la Ngwata (32)
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu kusini
wamepata pigo baada ya kumpoteza kada wao Mhamasishaji Erasmo
Nyindi ambaye amepata ajali katika Wilaya ya Nyasa
Mkoani Ruvuma akiwa katika ziara ya kazi .
Mtendaji
Mkuu wa kanda ya Nyanda za Juu Kusini Rajabu Kaluwa amesema baada ya kumulikwa
taa na watu wenye silaha, Dereva alishindwa kuliongoza Gari na kusababisha
Ajali iliyoua mtu mmoja Mhamasishaji Erasmo Nyindi na majeruhi watatu akiwemo
mgombea Ubunge kupitia ukawa na watu wawili ambao hali zao ni mbaya wako
Hospitali ya Litembo wakipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment