Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya amesema Serikali
inawathamini wafanya Biashara wanaoungana na Serikali katika kutatua Matatizo ya wananchi kuwa ni wafanya Biashara werevu.
Mkuu wa Wilaya ya
Songea Benson Mpesya amewataka wafanya biashara wajue kuwa Serikali inatambua
kuwepo kwa wafanya biashara hasa pale wanapoungana na serikali kuwasaidia
Wananchi wanapopatwa na Majanga.
Mkuu wa Wilaya ya
Songea Benson Mpesya ameyasema hayo alipokuwa akipokea bati 112 na misumari ya
bati kutoka kwa wafanya biashara wa manispaa ya Songea kwa lengo la kuwasidia
wananchi walioezuliwa Nyumba zao na upepo mkali ulioambatana na mvua na
kuziacha familia 15 bila kuwa na mahali pa kulala.
Mkuu wa Wilaya ya Songea akielekeza jinsi yakuimarisha nyumba kabla ya kuezeka amesema haraka haraka au mtu kutaka nafuu ndicho chanzo cha nyumba kuezekwa tofauti. Amesisitiza kuwatumia wahandisi kabla ya kuezeka ,Wahandisi hulipwa Mshahara kwa ajili ya kuwasaidia wananchi elimu waliyonayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea akipewa Maagizo na Mkuu wa Wilaya jinsi ya Kuwa saidia watu wanao ishi pembezoni ili waweze kuepukana na Majanga, amesema njia moja wapo ni kuwatembelea mara kwa mara na kuona kazi za maendeleo wanazozifanya zifanyiwe marekebisho kabla ya Madhara kutokea.
Mwenyekiti wa Wafanya Biashara Mkoa wa Ruvuma Issack
Mbilinyi (Mwilamba) amesema wafanya biashara ni moja ya Jamii, hawawezi kuona
watu wanateseka na wao wana pesa wakashindwa kusaidia Jamii bora ni ile
inayosaidiwa katika Matatizo.
Watu wa kijiji cha Nakahegwa wakichukua bati za msaada walizo letewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya
Mkurugenzi Mtendaji wa Hlimashauri ya Wilaya ya Songea Sixbet Valentin akiwa na Kaimu Mkurugenzi Weniselia Swai wakibadilishana mawazo ya kuweza kuimarisha uchumi pamoja na kuangalia upandishaji wa mazao ya biashara kama Mahindi,Kahawa na Maharage.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nakahegwa Songea Vijijini Damiani Sanga akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Beson Mpesya na kutoa shukurani kwa msaada wa Bati walio pewa wananchi wake
Wahanga waliopatwa na Matatizo ya kuezuliwa Nyumba zao katika Kijiji cha Nakahegwa waligala gala chini kushukuru kwa msaada waliopewa na kusema kweli huu ni Utawala wa sasa kazi
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya akiwa na familia ya Mzee Golihama wahanga wa kuezuliwa nyumba zao huko katika kijiji cha Nakahewgwa Songea Vijijini. kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Sixbet Valentine na katikati ni wahanga walioezuliwa nyumba zao Bibi Maria njovu na kijana wake John Matias Goliama.
Kiongozi bora ni yule anayepaswa kufuatilia kwa karibu matatizo ya wananchi wake anaowaongoza na kushiriki katika kuyatatua. Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Sixbert Valentine akiwa na watoto wa wazazi waliopatwa na maafa ya kuezuliwa nyumba zao kwa mvua iliyoambatana na upepo katika Kijiji cha Nakahegwa Songea Vijijini ambapo mkurugenzi aliwapa kiasi cha fedha ili wanunue daftari za shule kufidia daftari zilizoharibika kwa kunyeshewa na mvua.
Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa
ambao unapata Mvua nyingi zinazoambatana na upepo mkali, Mkuu wa wilaya ya
Songea Benson Mpesya amewataka wahandisi wa serekari Songea kutembelea wananchi
na kuwaelekeza jinsi ya kulinda nyumba zao na upepo kwakufunga Tengo zinazozuia
upepo badala ya kuwaacha wakizuia upepo kwa kufunga nyaya za matairi ya Magari.
Baadhi ya nyumba zilizopatwa na maafa ya kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua katika kijiji cha Nakahegwa kata ya mbinga Mwalule Songea Vijijini.
No comments:
Post a Comment