|
Mungu ndiye mwanzilishi wa kuchagua Viongozi, tunaambiwa mtu wa kwanza aliyetawala Dunia alikuwa Adamu. Utawala wa Adamu ulikuwa wa huruma, Ukatili ulianza pale mtoto wa Adamu Kaini alipomuua Habil. Hivyo hivo tunaona Utawala wa Yusufu alikuwa mdogo na nduguze waliamua kumuuza mdogo wao lakini ndiye aliyewaokoa wakati wa njaa. Hebu tuone Daudi naye alikuwa mtoto mdogo kazi yake kazi yake kubwa ilikuwa kuchunga lakini Mungu alipotaka kuweka mtawala aliamua kumteua Daudi. Sasa ninachotaka kusema ni jinsi gani Mungu ameweza Kumteua Dr. John Pombe Magufuli kuwa Rais, ni mfano wa Manabii waliopita, kazi ya Mcha Mungu kuwaonea huruma watu wanaoteseka. Hata Yesu alipofika Hekaluni alikuta Mafarisayo wakifanya Hekalu la mungu kuwa Soko. Lakini alimwaga vitu vyote na alisema msifanye Nyumba ya Mungu kuwa Soko la Wanyang`anyi.
Hivyo hivyo Rais Magufuli
wakati wa kumwapisha Waziri Mkuu Majaliwa Kasim, watu walichanga fedha shilingi
milioni 225 ili wafanye Sherehe lakini Rais akaamua kuzipeleka Fedha hizo
katika Hospitali ya Taifa ya muhimbili na kuwezesha kununua Vitanda, Magodoro
pamoja na shuka, suala kama hilo linahitaji ujasiri.
Hotuba yake aliyoitoa katika
Bunge la 11 ameeleza jinsi fedha za Serikali zilivyokuwa zinashindwa kutumika
ipasavyo kwa wanyonge, ambapo fedha nyingi zilitumika pasipokujali matatizo ya
watanzania. Fedha zilizotumika kwa safari za nje zingeweza kufanya mambo
makubwa.
Sasa jee? Mtu katoka CCM ni
mchaguliwa wa CCM waliokuwa wanafuja fedha ni viongozi hao hao wa CCM. Anapowafichua Mafisadi, wala
Rushwa tegemeo lake
ni nini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
kwa hivi sasa anasali sala ya Yesu Msalabani akisema Eloi, Eloi Lamasabakisani,
Mungu wangu Mungu wangu kwa nini unaniacha.
Watanzania tujue kuwa Sala
hiyo ni sawa wanavyosema Waislamu Ihidina Sita la Mstakimu Silataladhina Ana mnta wala dhuarimu ghairimu maudhubi wala dhuarimu. Utuongoze katika njia
ya watu walionyooka na sio wale walio wakasirikia.
Ndugu zangu, ninachomaanisha
Mtu akiomba msaada hatuna budi kumsaidia, Rais wetu anataka silaha kali ya
kumsaidia. Vita hii sisi Watanzania wote tuingie madukani kununua Bunduki kuwa
Askari wa Rais Mteule wa Awamu ya Tano Dr. John Pombe Magufuli.
Silaha zinazotakiwa ni
mkristo kununua Biblia na kuomba kwa Bidii, na Muislamu kununua Kurani Tukufu
na kusimamisha sala tano ili Rais afanikiwe katika Vita hii.
Viongozi wanaojitoa kwa moyo
wote wanatakiwa kusaidiwa, Miaka zaidi ya 51 iliyopita tulikuwa tukiomba
kumpata Rais atakayewasaidia wanyonge, Siku ya kwanza Muhimbili alitoa Pochi
yake kutaka kumlipia Bili ya Matibabu Mgonjwa. Jee, hapo huoni kuwa hali hizo
zinamkera?
| | | | | | | | | | | | | | | |
|
|
|
Adam Nindi mkurugenzi wa Blog ya Songea Habri akiwa na Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli, hii ina maanisha viongozi wa juu walivyokuwa karibu na wananchi wote hata wadogo.
Rais awamu ya tano Dr. John pombe Magufuli kipenzi cha watanzania akishukuru kwa kumuamini kuongoza watanzani na kuwathibitishia kuwa kwake ni kazi tu.
Rais wa Awamu ya nne Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete amejitahidi kuiongoza Nchi mpaka kufikia hali hii
tuliyokuwa nayo, Ni nadra kiongozi anayetawala kuweza kukabidhi utawala kwa
Amani. Kwa wastani hakuna mtu
asiyekosea isipokuwa Mungu, Maksi ya Dr Jakaya Mrisho Kikwete ni kule kusimamia
Amani na Utulivu na ndicho kilio cha Walimwengu wote.
Picha ya hapo juu ni picha
inayoonyesha jinsi waandishi walivyokuwa wakiwajibika kutangaza habari za
kuweza kuiweka Nchi yetu katika Amani ili Uchaguzi uwe wa Haki na uhuru. Adam
Nindi M
Watanzania ni watu waliokuwa na msimamo wa kuendeleza na kuilinda Amani na utulivu kama inavyojieleza nembo hiyo hapo juu.
|
Rais Mteule wa Awamu ya Tano
alikuwa akitoa mfano wa wazi kuhusu Maendeleo ya Tanzania,
alisema barabara za lami zimejengwa wale ambao hawana magari wasingelijua hilo, akitoa mfano mdogo
kuwa katika simu unampigia mpenzi wako I Lovw You; hayo ni maendeleo
ukilinganisaha na wakati wa TTCL Unakaa foleni mpaka uipate laini kumekucha,
hapo Rais akipiga Simu.
|
Picha iliyo mbele yako ni
Adam Nindi akisalimiana na Rais wa awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa, hiyo ni
ishara ya kuwa Viongozi wa Tanzania wanawajali watu wadogo, Adam Nindi na Rais Mkapa wapi na wapi lakini
huo wote ni upendo.
Adam Nindi akimuuliza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuhusu Madini yaliyopo Mkoa wa Ruvuma,
Watanzania watafaidika vipi kwa kuwa Mikoa yenye Madini mara zote watu wake
wanakuwa wa kwanza kufaidika.
Adam Nindi akiwa na Rais
Karume wa Zanzibar
akimuuliza akiuliza jinsi gain atakavyosimamia Muungano wa Zanzibar baada ya kuona watu wachache
wakiubeza Muungano, lakini Rais Karume alikuwa imara aliongoza vizuri na mpaka
anatoka Muungano ameuacha imara.
No comments:
Post a Comment