Serikali Wilayani Songea Ruvuma imetoa
pole kwa Wananchi waliopatwa na
Maafa baada ya Nyumba zao kuezuliwa na Upepo ulioambatana na Mvua kali
Mkuu
wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya amesema Kamati ya Maafa Wilaya ya Songea baada ya kuona hali mbaya ya Kaya 8 aliona ni
bora ianze na kaya hizo, akitoa msaada huo alieleza nia ya serikali kwa
wananchi wake wakati akimkabidhi bati Christina Kambanga wa Mtaa wa Namanyigu Kata ya mshangano.Maafa baada ya Nyumba zao kuezuliwa na Upepo ulioambatana na Mvua kali
Mhandisi wa Ujenzi Manispaa ya Songea akihakiki Bati wakati wa kukabidhi kwa waathiriwa walioezuliwa nyumba zao.
Kamati ya Maafa Wilaya ya Songea imeweza kukabiliana na Janga la kueziliwa kwa nyumba za baadhi ya wananchi wake kwa kutoa Msaada kwa kaya 8 ukiwa na Thamani ya Shilingi 1,050,000.
Baadhi ya Nyumba zilizoezuliwa Kata ya Mletele Manispaa ya Songea, kama inavyoonekana bati zikiwa zimetupwa mbali na upepo ulioambatana na mvua iliyonyesha tar 1/11/2015
Kama inavyoshuhudia nyumba ikiwa imeezuliwa paa katika Eneo la Mtaa wa Unangwa kata ya Seed Farm Manispaa ya Songea.
Nyumba ikiwa ilivyoezuliwa paa Kata ya Seed Farm.
Wananchi waliopata Msaada huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Unangwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Maiko Mpangala amesema kauli ya mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli ya kusema hapa kazi tu, imethibitika baada ya wananchi kupatwa na janga la kuezuliwa nyumba zao,k iliyoungwa mkono na waliopatwa na Maafa hayo. | |
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya akieleza Hali halisi ya Uharibifu huo, na kuainisha gharama ya msaada uliotolewa na Kamati ya Maafa
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya amesema mara nyingi jamii inapopatwa na janga inakuwa haina jinsi ya kufanya ila hukabilianana janga hilo kwa kuchangishana baadhi ya garama ama huishia kukata tamaa.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesiya akitoa pole amesema Manispaa yaSongea imepatwa na Janga hilo ambapo Nyumba zaidi ya 15 zimeezuliwa.
No comments:
Post a Comment