Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ruvuma wamesema wanapinga vikali kuteuliwa Zubeda Hassan Sakuru kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Wanachama wa BAWACHA Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wametoa Tamko la pamoja, wapo tayari kutoka CHADEMA endapo uteuzi huo hautabatilishwa wamesema Zubeda Hassan Sakuru siyo mkaazi wa Mkoa wa Ruvuma hata wilaya waliyo sema ana toka Tunduru hakuna hata mmoja anaye mjua . Jambo waliyo baini nikuona chama kipo mkononi mwa mtu mmoja.
Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wakiwa ndani ya Ofisi za CHADEMA wilaya walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko la kupinga Uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalum atakayewakilisha Mkoa wa Ruvuma uliofanywa na Uongozi wa CHADEMA Taifa.
Wanawake wa CHADEMA kutoka wilaya za Tunduru, Nyasa, Mbinga, Namtumbo, Songea Vijijini na Songea Manispaa walipokutana katika Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea kutoa TAMKO hilo.
wanachama wa Chadema wakiwa nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya Matarawe Manispaa ya Songea mara baada ya kutoa Tamko la Kupinga Uteuzi huo wa Mbunnge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Wanachama wa BAWACHA nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea Mjini.
Wajumbe wa BAWACHA kutoka wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment