Nchi ya Tanzania
ni nchi ya 91 kati ya Nchi 96 Duniani kwa Wazee kuwa katika hali hatarishi kwa
maisha ya wazee kwa kukosa mahitaji muhimu ikiwemo afya, Elimu Chakula na
Malazi.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa ameyasema
hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma
katika kutafuta njia ya kuwakwamua wazee waweze kutokana na hali hiyo.
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma
wameazimia kuifahamisha Serikali kujua kuwa haki ya Kuishi pamoja na huduma nyingine
ni wajibu wa Serikali kuwatekelezea Wazee.
Mkurugenzi wa shirika la PADI linalohudumia wazee Nchini
Tanzania Iskaka Msigwa amesema Tanzania
ina wazee wapatao milioni 2.5, wanawake wakiwa milioni 1.3 na wanaume milioni
1.2. Idadi hiyo ya wazee ndiyo inayohudumia Watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi na kupelekea wazee hao kuambukizwa magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo
Ugonjwa wa UKIMWI.
Waqandishi wa Habari wakijadili jinsi ya kunusuru Maisha ya Wazee kuhusiana na Changamoto zinazo wakabili
Aidha Wazee wanatakiwa wapewe kipaombele kama
ilivyo kwa Wanawake kuwa na Wawakilishi katika viti Maalumu vya Ubunge na
Udiwani, vivyo hivyoi na Wazee wanatakiwa wawe na Viti Maalumu vinavyowakilisha
wazee.
Moja ya Wazee ambao wana tegemea kinga kutoka kwa jamii jinsi yakupata kinga ya tuhuma mbalimbali kutoka kwa watu wenye imani potofu.Wazee wanalia na Pesheni ya kuweza kupata fedha ingawa kidogo tu
Katika Kikao hicho imebainika kuwa huduma za Wazee zinashindwa kutekelezawa kutokana na kutokuwa na wawakilishi katika Vyombo vya Maamuzi kama
No comments:
Post a Comment