Mapadre na Maaskofu mbalimbali wamepongeza hatua ya Uongozi wa Makanisa ya Anglikan kwa kupinga Ndoa za jinsia moja kinyume na maadili ya kiAfrika wameahidi kuunga mkono jitihada za kulaani kuruhusu uhalali wa ndoa hizo.
Katika Ibada ya Umoja wa makanisa ndugu mwaka Huu waumini wa Makanisa ya Moravian KKKT, RC na Anglikan mkoani Ruvuma wamemshukuru Mungu kwa kuwezesha Tanzania kumaliza zoezi la Uchaguzi mkuu kwa amani bila kuvuruga amani ya Tanzania.
Umoja wa Makanisa Ndugu Mkoa wa Ruvuma umepinga Vikali Biashara haramu ya Binadamu inayofanywa na watu wachache wenye uchu wa uchumi wa haraka haraka.
Katibu wa akina Mama wa Umoja
wa Makanisa ndugu Mkoa wa Ruvuma Imelda Mbawala amesema kumeibuka Biashara ya Binadamu ambapo Mkoa wa
Ruvuma unashika nafasi ya tatu kwa kuuza binadamu kwa usiri mkubwa, Amesema Makanisa
yana ushahidi baada ya familia moja kutoroka katika Nchi zinazofanya
biashara hiyo .
Katibu wa Akina Mama wa Umoja
wa Makanisa ndugu Songea Imelda Mbawala ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha siku 9 za maombi ya pamoja ya kuombea amani na kulaani Vitendo vya Ukatili dhidi ya Binadamu, ikiwemo biashara haramu ya binadamu na kupinga ndoa za jinsia moja, Ibada iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya
Ruvuma Ushirika wa Songea na kushirikisha Makanisa 4 ya Kikatoliki, 2 ya KKKT, Moravian na makanisa 2 ya Anglikan.
Waumini wa Kanisa la Moravian manispaa ya Songea wakimsifu Mungu katika Ibada hiyo ya pamoja ambapo wamekemea roho za ujasusi zikiwemo za Alishababu, na vitendo vya kuashiria uvunjifu wa amani.
Waumini wa Kanisa Katoli Jimbo kuu la Songea wakiwa katika Ibada ya pamoja ya Umoja wa Makanisa Ndugu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Manispaa ya Songea.
Alipo ulizwa Kaimu Kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi kwa njia ya simu kuhusu uwepo wa biashara haramu ya binadamu mkoani Ruvuma, alisema jeshi la Police lina fanya uchunguzi kuhusu suala hilo
Lengo la makanisa kuungana pamoja na kufanya ibada za pamoja ni kudumisha umoja na kuondoa tofauti zilizopo kati ya kanisa na kanisa kwa kuwa mungu ni mmoja ambapo katika umoja huo hufanya maombi ya pamoja ya kuliombea Taifa, Viongozi wa Serikali na Mambo yanayoikumba Jamii.Waumini wakitafakari Neno katika ibada ya pamoja ya kuiombea Amani ya Tanzania.
Naye Padre Turdo Chuma akitoa mahubiri ameupongeza Uongozi wa Makanisa ya Anglikana kwa kupinga Ndoa za Jinsia moja kinyume na maadili ya kiafrika, amesema wanaunga mkono kwa kuwawekea vikwazo Makanisa ya Marekani yanayounga mkono ushoga
Mapadre na Wachungaji wa makanisa ya Kikatoliki, Moravian, KKKT na Anglikana wakiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Padre Nicodemu mbano wa kanisa Katoliki la mtakatifu Mathias Mlumba kalemba Jimbo Kuu la Songea katika Ibada ya pamoja kuhitimisha wiki ya Maombi ya pamoja duniani.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Ruvuma, Askofu Amon Mwenda kulia akiongoza waumini wa umoja wa Makanisa ndugu katika Ibada ya pamoja iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Songea, katikati ni Naibu Askofu wa KKKT Mchungaji Laurent Ngaoneka
Bi Helena Kawinga Muumini wa Kanisa la Anglikan Songea Mjini akisoma Somo la kwanza katika Ibada ya Umoja wa Makanisa Ndugu.
Waumini wa makanisa ndugu Songea wakiwa katika ibada ya pamoja kuhitimisha siku 9 za ibada ya pamoja.
Waimbaji wa kwaya ya Romanic Katholiki Jimbo kuu la Songea katika Ibada ya umoja wa makanisa ndugu
Waimbaji katika maombi ya pamoja wakimsifu mungu.
Katika ibada hiyo ya pamoja waumini waliweza kuombea wagonjwa wanaohangaika na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano ajaliwe utawala bora katika kipindi chake
Umoja wa Makanisa Ndugu Mkoa
wa Ruvuma umefanya Ibada kwa siku 9 kwa
kupitia kila Kanisa kuombea Amani na kumalizia Kanisa la KKKT kwa kulaani
Biashara haramu ya Binadamu na kukemea Ndoa za Jinsia moja.