KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, January 3, 2016

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGAN WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASIMU MAJALIWA AMEWATAKA WANA RUVUMA KUPIGA VITA UKIMWI



ADAM NINDI ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI RUVUMA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa amewataka wana Ruvuma kuangalia upya jinsi ya kuweza kukabiliana na Maambukizi ya UKIMWI amesema takwimu bado zinaonyesha kuwa maambukizi bado yapo juu kimkoa kwa asilimia 7%

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa ameyasema hayo baada ya kupokea tarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu akieleza hali ya elimu , uchumi na Afya

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa amesema jambo lakusikitisha ni kuwa ugonjwa huo wa UKIMWI unawakumba vijana zaidi kuliko ilivyozoeleka kuwa wazee ndio wenye maambukizi, vijana kati ya umri wa miaka 19 na miaka 29 ndio wenye maambukizi ya UKIMWI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa amesema jambo hili lisipopata ufumbuzi linaonyesha siku zijazo tutakosa nguvu kazi ambayo ni vijana.

Akizungumzia upande wa Uchumi amesema, Mkoa wa Ruvuma uko mbele kiuzalishaji wa Chakula pia pato la mtu mmoja mmoja limekuwa kutoka laki sita kwa mwaka hadi kufikia milioni mbili kwa mwaka huu ni ufaulu mkubwa alisema,

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa ametoa angalizo kwa Halmashauri amesema sasa wanatakiwa kutazama upya kuhusu upimaji wa Aridhi wawasaidie Wananchi kuwapimia Ardhi kwa bei nafuu wasiangalie Mapato waweke uzalendo zaidi. Kuweka kiasi kikubwa ni kuwakosesha Ardhi yao Wazawa halafu wanafaidika wawekezaji

Akizungumza kuhusu kiwanda cha SONAMCU Kilichokuwa kikisindika Tumbaku amesema atafanya mazungumzo na viongozi wa ushirika huo aone jinsi ya kuweza kukifufua kiwanda hicho

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akiwa ziarani mkoani Ruvuma anatarajia kufanya ufunguzi wa tawi la benki ya posta, kukagua ghala la Taifa la hifadhi ya chakula NFRA, Kukagua ujenzi wa Makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Songea, Kukagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (HOMSO)
 Waziriri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akitelemka kwenye ndege wakati akiwasili mkoani Ruvuma na Kupokelewa na Maelufu ya wana Ruvuma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu uwanja wa Ndege Songea
 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Leonidas Gama akisalimiana naWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Vijana wa Chipkizi wa CCM wakimvisha Skafu  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akimsogelea Katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Magret Malenga
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa akisalimiana na Jaji wa Kanda ya Songea
 Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela akisalimiana naWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Afisa uhamiaji Mkoa wa Ruvuma akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa katika kiwanja cha ndege cha Songea kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Mmoja wa wanakamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Ruvuma akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Naibu kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Chiristophe Myava  akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini Mpakate Mpakate akisalimiana naWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwana
 Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea  Raphael Kimary akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
 Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika kiwanja cha ndege cha Ruhuwiko Songea kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa
Afisa wa Jeshi la Police Mashimbi akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa

No comments:

Post a Comment