Mh. Waziri wa Afya akizindua mpango wa Madaktari Bingwa wanaotoa huduma mikoani kwa mkataba wa muda mfupi ili kuwasaidia wagonjwa wanaopata rufaa za kutakiwa kutibiwa hospitali kubwa, amewaagiza watu wa Bima Afya waangalie uwezekano wa kutoa huduma hiyo mara mbili kwa mwaka mikoani ili kuwafikia wahitaji wengi ambao hawana kipato cha kuwafikisha katika Hopitali kubwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto akisikiliza maelezo ya Mtoto mwenye tatizo la ugonjwa wa Moyo katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiongea na wagonjwa na wauguzi waliokuja katika Hopitali ya Mkoa Songea wakati akiwa katika Ziara ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kujionea hali ya utoaji wa huduma na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.
Ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ilibaini upungufu wa baadhi ya Vifaa tiba katika Kitengo cha upasuaji. Sambamba na hilo akiwa peramiho aliupongeza uongozi wa Hospitali kwa kupiga hatua ya kutengeneza Dawa za majimaji Drips ambapo kwa siku ina uwezo wa kuzalisha lita 250 za Ddrip amesema Tganzania ina nafasi kubwa ya kuacha kuagiza dawa nje kama hospitali ya peramiho inafanya kwa nini Muhimbili Hospitali kubwa iagize Drips toka Nje ya Nchi.
Katika Ziara yake mkoani Ruvuma Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alitembelea Ofisi za Dawati la Jinsia la Polisi Wanawake na kupokea taarifa ya uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi za Dawati la Jinsia la Polisi.
Mwenyelkiti wa Dawati la Jinsia la Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo akimweleza Waziri wa Afya uendeshaji wa Dawati la Jinsia na changamoto wanazokutana nazo katika kushughulikia kesi za Kijinsia ikiwemo na kukithiri kwa ongezeko la uwepo wa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu
Katika Ziara ya waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa Mkoani Ruvuma alipata fursa ya kuongea na Wazee kupitia Shirika la PADI linalohudumia Wazee. Pichani ni Mwenyekiti wa Baraza Huru la Wazee Manispaa ya Songea Lenzian Nyon akisalimiana na Waziri Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto amewaagiza uongozi wa Hnospitali ya Misheni ya Peramiho kucha kuwatoza gharama za matibabu wanawake na watoto badala yake wafuate Sera ya Afya inavyosema Matibabu bure kwa Wazee, Wanawake na Watoto pia wazee watengewe madirisha maalumu na Daktari wa kuwasaidia kwa kuwa Hospitali hiyo imeingia mkataba na Serikali kama hospitali teule ya Wilaya. Pichani Waziri akiagana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa Bima ya Afya Maiko Mhando na viongozi wengine katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Songea, wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum wanawake Mkoa wa Ruvuma Jacquelin Ngonyani Msongozi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu kulia akiongoza msafara wa kumsindikiza Wari Ummy Mwalimu baada ya kumaliza Ziara yake katika Wilaya ya Songea na Manispaa ambapo alitembelea Hospiktali ya Mkoa, Hospitali ya misheni ya Peramiho, hospitali ya wilaya Mjimwema, Dawati la jinsia na kumalizia na kuongea na wazee muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa Ndege wa Songea.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu akipanda Ndege katika uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Songea baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment