Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka Walimu wa Shule za
Msingi na Sekondari kuacha kumfukuza Mmwanafunzi kwa ajili ya kukosa kulipa
Michango ambayo wamekubaliana wazazi wenyewe.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameyasema hayo baada ya
wazazi kumlalamikia kuendelea kwa michango ya nyuma ambayo ilikuwa ya walinzi pamoja na
chakula
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu amewataka wazazi wajue
kuwa Serikali imetoa msamaha wa ada na siyo wazazi kuwaacha watoto na njaa
shuleni ni juu yao
kuhakikisha watoto wanapata chakula.
Afisa Elimuj Manispaa ya Songea Edith Malata Kangomba amesema katika suala la kuandikisha watoto
wenye ulemavu limeeleweka kwa wazazi kwa mwaka huu zaidi ya watoto 200
wameandikishwa ukilinganisha na zamni walivyokuwa wakifichwa majumbani.
Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Lilambo Osmundi
Mwingira ameomba mwongozo kwa Serikali kwa kuwa Wananchi wanadai michango yao ya chakula baada ya
Serikali kusema hakuna Michango.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Jenifa akifafanunua jinsi alivyo jipanga kudhibiti swala la michango mashuleni
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
amesema ni marufuku Walimu wakuu kushiriki katika kudai
Michango ambayo Serikali imekataza, suala la michango ya
chakula kuboresha majengo isimamiwe na Wananchi wenyewe kwa kutumia kamati za shule bila kumuathiri
mwanafunzi.
No comments:
Post a Comment